AFISA TAKUKURU IRINGA AMPIGA KOFI MWALIMU MJAUZITO KISA DAFTARI LA MAHUDHURIO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 2 December 2020

AFISA TAKUKURU IRINGA AMPIGA KOFI MWALIMU MJAUZITO KISA DAFTARI LA MAHUDHURIO

Katibu wa Chama cha Walimu 
(CWT), Wilaya ya Kilolo, Anthony Mang’waru akiongea na waandishi wa habari juu ya sakata la kupigwa kwa mwalimu.

Na Fredy Mgunda, Iringa

CHAMA cha Walimu Wilaya ya Kilolo kimeanzima kutoshikiana na taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa kutokana na madai kuwa mmoja ya maafisa wake kupiga mwalimu wa shule ya msingi Kitelewasi akiwa kwenye majukumu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kilolo Mtemi Mgalula  alisema kuwa wamefedheheshwa na kitendo cha afisa TAKUKURU kumpiga mwalimu  kibao akiwa anatekeleza majukumu yake akiwa kazini.

Alisema kuwa wameanzimia kumpeleka mahakamani afisa huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho alicho kifanya kisichokuwa cha uungwana kwa mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Kitelewasi.

Mgalula aliongeza kuwa wameanzimia kutoshirikiana kwa jambo lolote lile na taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwazalilisha walimu wawapo kazini.

“Hakuna jambo au tukio lolote ambao walimu wa wilaya ya Kilolo watashirikiana na taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa hadi pale watakapojirekebisha na kuacha kuwanyanyasa walimu wawapo kazini” alisema

Mgalula alisema kuwa wataanza kutoa elimu ya walimu kujilinda kwa kuwa sheria za nchi zinarusu kujilinda ili waache kunyanyashwa na kufanya kazi yao kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao na kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Hakuna haki ya mwalimu huyu itakayopotea kwa kuwa tunajilinda na tunaviongozi wa mkoa ambao wanathamini kazi za walimu hivyo tunauhakika kuwa mwalimu huyu atapata haki yake na huyo afisa tunamkaribisha aje tuongee lakini lazima haki ya mwalimu ipatikane.

Akieleza tukio hilo mwalimu Latifa Kitosi ndiye anayetajwa kupigwa na afisa TAKUKURU alisema kuwa maafisa hao walifika ofisi na kuomba daftari la mahudhurio ya darasa la sita la mikondo yote miwili lakini kwa halaka daftari la mahudhurio lililokuwepo jirani ni daftari la mkondo B wakati mahitaji ya maafisa hao wa TAKUKURU walikuwa wanahitaji daftari la mkondo A

Alisema kutokana na daftari la mkondo A yaliibuka majibizano baina ya maafisa hao wa TAKUKURU na walimu waliokuwepo katika ofisi hiyo na mmoja ya maafisa hao kupiga kibao mwalimu ambaye ni mjamzito na kisha kulichukua daftari hilo la mahudhurio na kumtaka mwalimu huyo kufika katika ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa mahojiano zaidi.

Kitosi alisema kuwa maafisa hao walimtuhumu yeye na mwalimu mkuu msaidizi kuwa kuharibu ushahidi wa mahudhurio ya mwanafunzi  kutokana na kuchelewesha daftari la mahudhurio la mkondo A ambalo hasa maafisa hao walikuwa wanalihitaji kwa ajili ya kuangalia mahudhurio ya mmoja ya wanafunzi wa darasa hilo.

Aliongeza kuwa chanzo cha hayo yote yanatokana na mwanafunzi kutohudhuria masomo kwa kipindi cha siku kumi na nne bila taarifa yoyote ile kwa uongozi wa shule hiyo ya kitelewasi.

Kwa upande wake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Chako Mdemu alisema kuwa mnamo  tarehe 12 alipata ujumbe mfupi ukieleza kuwa kuna kila dalili za kutoroshwa kwa mwanafunzi huyo kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kama ambavyo imekuwa ikifanyike kwa wanafunzi wengine walivyokuwa wanafanya miaka ya zamani.

Mdemu alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo ndipo walipotoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ili kuweza kuzuia kutoroshwa kwa mwanafunzi huyo wa darasa la sita katika shule ya sekondari ya Kitelewasi wilayani kilolo mkoani Iringa.

Mwalimu mdemu alisema kuwa kuanzia mzazi wake,dada yake na mwanafunzi mwenyewe walikiri kuandaa mikakati ya kumtorosha mwanafunzi huyo kinyume na sheria za nchi na ndio kilikuwa chanzo cha dada wa mwanafunzi huyo kupeleka keshi hiyo TAKUKURU.

Alisema kuwa maafisa hao wa TAKUKURU hawakuwa wamejitambulisha wala kuandikisha kuwa wao ni maafisa TAKUKURU hivyo ili kuwa ngumu kwa viongozi wa serikali ya kijiji na walimu kuwatambua kuwa wao maafisa wa serikali na wameenda kwa kazi maalum.

Naye kamanda wa taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa,Domina Mkama akiri kupigwa kofi kwa mwalimu huyo wa kike ambaye ni mjamzito kutokana na mazingira ambayo walimu hao walikuwa wamemtengenezea afisa huyo hadi kutokea tukio hilo.

Mkama alisema baada ya kupigwa kofi mwalimu huyo ndio daftari la mahudhurio lilitolewa na huyo mwalimu na kuendelea na upelezi ambao maafisa hao walikuwa wanauhitaji kwa ajili ya kuifanyia kazi ambayo walikuwa wanataka kuifanya.

Alisema kuwa serikali kwa serikali hawawezi kugomba hivyo ameumba uongozi wa chama cha walimu wilaya ya Kilolo kukaa meza moja kuhakikisha wanalimaliza tatizo hilo mara moja ili kuendelea kushirikiana kama ilivyokuwa hapo awali.

Lakini pia katibu wa CWT wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru alisisitiza kuwa hawataendelea kutoa ushirikiano na taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa hadi pale watakapo kaa meza moja na kufikia muafaka na kusitisha vitendo hivyo vya kuwanyanyasa walimu.

Tumesikitishwa sana na tunalaani kitendo hicho cha kupigwa kwa mwalimu na kitendo ambacho sio cha kiungwana kufanya tukio hilo na ambacho hakikubariki kabisa kwenye jamii yeyote ile hapa nchini.

 

 

No comments:

Post a Comment