KATIKA kuunga mkono jitihada za uthibiti wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini, leo ikiwa Siku ya Ukimwi duniani, Benki ya NMB imetoa msaada wa tisheti zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho mjini Moshi na elimu kuhusu umuhimu wa kukata bima ya afya.
Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela - PrayGod Godwin akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro - Anna Mghwira Msaada wa Tisheti zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniania leo ofisini kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko(kushoto) akizungumza na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini-Aikansia Muro (Kati), Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela - PrayGod Godwin na Meneja Mwandamizi Huduma za Serikali - Christabel Hiza mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment