Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya
Meya wa Jiji la Tanga.
Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.
Meza
kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uchaguzi huo katikati ni
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia ni Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza na waheshimiwa madiwani kabla ya kuanza uchaguzi huo.
Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akiwa na Mstahiki Meya mpya
wa Jijini la Tanga (CCM) Abdurahaman Shillow kushoto na anayefuatia ni
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Jiji la Tanga.
Ummy ameyasema hayo katika kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya
Meya wa Jiji la Tanga ambapo ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha na
wananchi wa Tanga Mjini wamewaamini kwa kuwapa ushindi mkubwa kwa
mgombea Urais, Ubunge na Madiwani wa CCM katika kata zote 27 za Tanga
Mjini.
Alisema baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi hao wana wajibu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga mjini bila
kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Mhe
Ummy amempongeza Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow kwa kuaminiwa kuwa Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga huku akihaidi kumpa ushirikiano wakati wote wa
utekelezaji wa majukumu yake.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa
Tanga ulisimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
No comments:
Post a Comment