UWAMAKIZI NI CHUO CHA UTUNZAJI MAZINGIRA DUNIANI-JENERALI MSTAAFU MWAMUNYANGE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 18 October 2020

UWAMAKIZI NI CHUO CHA UTUNZAJI MAZINGIRA DUNIANI-JENERALI MSTAAFU MWAMUNYANGE

 _MG_6851 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya mafunzo mara baada ya kufika Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly.


_MG_6712
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dk. Ally Fungo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.


_MG_6738
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja.


_MG_6798
Sehemu ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) wakifuatilia maelezo kuhusu namna ya uhifadhi wa mazingira kutoka kwa Mtaalamu wa Mazingira Tanga Uwasa Ramadhani Nyambuka.


_MG_6896
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly katikati akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kushoto wakati wa ziara hiyo kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja wa kwanza kushoto ni 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo.

_MG_6903
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara hiyo wa pili kutoka kulia aliyevaa shati jeupe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo.

_MG_7017
Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akieleza namna wanavyotunza mazingira katika vyanzo vya maji kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Dawasa wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.

_MG_6956
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja.


_MG_6958
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akitoka kwenye maeneo ya uhifadhi ya Uwamakizi wakati wa ziara hiyo.

_MG_6899
Maji yakitiririka kutoka kwenye bwawa la mabayani.


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na umoja wa wakulima wahifadhi wa Mazingira Kihuwi (Uwamakizi) huku akieleza hicho ndio chuo kikuu cha utunzaji wa mazingira sio kwa Tanzania  bali Afrika na hata Dunia.

Huku akiwataka watu waje kuona namna hatua wanazozichukua kuweza kutunza vyanzo vya maji uhifadhi mazingira ambao umekuwa na tija kubwa kwa kushirikishi wananchi ambao wamekuwa wakiishi karibu na maeneo yaliyokuwa na vyanzo hivyo.

Mwamunyange aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yao ya kimafunzo ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) ambapo walitembela maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Bustani ya Uwamakizi katika mlima wa mfano wa shughuli za uwamalikizi,

Maeneo mengine ambayo walitembelea ni eneo la uhifadhi wa mto Mihale katika mpaka unaotenganisha kijiji cha Kimbo na Shembekeza vilivyipo kwenye kata ya Kisiwani na Potwe wilayani Muheza na Bwawa la kuhifadhi Maji la Mabayani.

Alisema wamefurahishwa sana na dhana hiyo ya Uwamakizi kwa sababu ni nzuri kwa sababu wamegeuza changamoto kuwa fursa nzuri kwa kutumia ubunifu na kuongeza vitu vipya kwa kuhakikisha wanatunza mazingira

 “Kwa kweli nimefurahishwa sana na ubunifu huu sikutarajia ningeuona hapa niwapongeze sana muendelee hivyo na ari na moyo wa ushirikiano muendeleze upendo na amani maendeleo yetu yanatakiwa kuletwa sisi wenyewe ”Alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi.

Alisema walisikia sifa nyingi kuhusu juhudi na kazi nzuri waliyoipata katika utunzaji mazingira na vyanzo vya maji baada ya kusikia sifa hizo wakasema ni vuzuri wao kama bodi waje wakajionee wenyewe hizo sifa zinatokana na nini isije kuwa maneno.

Aidha alisema hivyo wakawaomba Tanga Uwasa kwa ajili ya bodi kuja kujionea wenyewee hayo yote na walifika na wakaanza mazungumzo nao baada ya maelezo wakafika kwenye baadhi ya maeneo kujionea wenyewe huku wakihaidi kwenda kuwa mabalozi wao.

Awali akizungumza kabla ya kuanzia ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo aliwakaribisha huku akieleza kwamba hiyo ni heshima kubwa kwao na wameona kuna kitu wanakikosa ambacho watawaonyesha

Aidha alisema ni madhumni yao ziara kama hizo sio hii ya pekee bali ziweze kuwa nyingi ili waweze kushirikiana kila fursa itakapojitokeza na kila wakati itakapohitajika.

“Katika ziara hii leo watatembelea bwawa la kuhifadhi maji mabayani,kijiji cha Mashewa kitongiji cha ikulu kuangalia uhifadhi wa kingo za mto na jinsi uwamakizi wanavyotumia mita 60 za uhifadhi wa mto,kutembelea ofisi za uwamakizi ,wakaona vikundi vya sanaa cha uhamasishaji uhifadhi wa mazingira na kuangalia eneo lilioandaliwa”Alisema Dkt Fungo

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema ziara hiyo ya mafunzo ni kujifunza namna ya utunzaji wa vyanzo vya maji ndio ambacho kimewafanya kuja kuona.

Akizungumza wakati wakiwa kwenye bwawa la Maji la Mabayani walielezwa namna wanavyotumia sheria ya mita 500 kwenye bwawa hilo ambalo linatumika kama chanzo cha maji.

Hata hivyo alieleza wana kijiji wanalinda wenyewe hata mtu akiwa anakata mti hapa anakutwa amezingizwa tayari hatua ambayo ilimfurahisha Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.

No comments:

Post a Comment