WAZIRI DK KIGWANGALLA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI DK WRIGHT KUZUNGUMZIA UTALII - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 7 September 2020

WAZIRI DK KIGWANGALLA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI DK WRIGHT KUZUNGUMZIA UTALII

 

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu mchango wa Taifa la Marekani katika shughuli za Uhifadhi nchini Tanzania na namna nchi yake itakavyoendelea kusaidia shughuli za uhifadhi katika eneo la Mafunzo, Teknolojia na Vitendea kazi  walipokutana kwa  mazungumzo jijini Dar es salaam.



Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) na ujumbe wake kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa, kudhibiti ujangili pamoja na Taifa kuendelea kunufaika kimapato, kutoa fursa za ajira na uwekezaji kwa Watanzania na Wageni akimwomba Balozi huyo asaidie kuhamasisha raia wa Marekani waje kuwekeza nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment