WAKUU WA IDARA NYASA WAPEWA MWONGOZO KURATIBU MAENDELEO YA WAVUVI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 10 September 2020

WAKUU WA IDARA NYASA WAPEWA MWONGOZO KURATIBU MAENDELEO YA WAVUVI

Wakuu wa Idara na vitengo wakiwa katika picha moja mara baada ya kumaliza kutoa maoni juu ya uratibu wa miongozo ya kimataifa yaliyotolewa na Wataalam toka Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa kushirikana na Shirika la kilimo na chakula Duniani FAO juu ya Uboresaji wa Sekta ya Uvuvi mdogo  Nchini. Picha na Ofisi ya Ded Nyasa.

    
Na Netho Credo, Nyasa

JANA katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, umefanyika Mkutano wa timu tendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wakuu wa idara na Vitengo, Mkutano wenye lengo, la kuchukua maoni ili kuendeleza Sekta ya Uvuvi Mdogo nchini kwa Muktadha wa kuhakikisha Usalama wa Chakula na kupunguza umaskini. 

Mkutano huo umeendeshwa na watalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na uratibu wa Shirika la Kilimo na chakula Duniani FAO ambao imeandaa mwongozo wa hiari, unaoelekeza misingi na masuala ya muhimu ya kuzingatia ili kurahisisha ushughulikiaji wa maendeleo ya sekta ya uvuvi mdogo katika nchi yoyote ulimwenguni.

Aidha washiriki walipata fursa ya kubainisha changamoto zinazowakabili wavuvi na kutoa suluhisho nini kifanyike ili wavuvi waboreshewe maslahi.vitendea kazi vya kisasa na kuwa na jamii yenye maendeleo.

Lengo kuu la kutekeleza mwongozo wa kimataifa unaohusu uvuvi mdogo ni kuhakikisha nchi yetu inatunza raslimali za uvuvi, kwa ajili ya kizazi cha sasa na kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya uvuvi yanaongezeka, na hivyo kuchangia katika kuhakikisha usalama wa chakula nchini na kuboresha hali ya uvuvi ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii yauvuvi.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Bernad Semwaiko alizitaja Baadhi ya changamoto zinazoikabili Sekta ya Uvuvi Wilayani hapa ni Ukosefu wa Zana za kisasa za uvuvi, kwa kuwa wavuvi wengi hutumia zana duni kwa ajili ya Uvuvi, Ukosefu wa elimu ya Uvuvi, kwa kuwa kwa sasa wavuvi wengi wanavua kama Utamaduni wa Kabila la Wanyasa.

Serikali kupitia Wizara ya mifugo na uvuvi inaratibu zoezi la kuandaa mpango kazi utakaotumika katika kutekeleza mwongozo huo wa kimataifa wa Uvuvi mdogo.


No comments:

Post a Comment