UZUSHI NA UWONGO WAMPONZA MGOMBEA, TUNDU LISSU, NEC YAMWITA...! - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 28 September 2020

UZUSHI NA UWONGO WAMPONZA MGOMBEA, TUNDU LISSU, NEC YAMWITA...!

Mgombea wa urais wa CHADEMA,  Tundu Lissu.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imemtaka mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufika mbele ya kamati ya maadili ya taifa kutoa ushahidi kuhusu madai aliyotoa dhidi yake kuwa kunaahujuma imepangwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Wilson Mahera Charles amesema kuwa Tume hiyo imesikitishwa na taarifa za uwongo, uzushi na upotoshaji zilizotolewa na mgombea wa urais wa CHADEMA,  Tundu Lissu siku ya Jumamosi, akisema kwamba Rais Dk. John Pombe Magufuli aliitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo yote jijini Dodoma kwa lengo la kuhujumu Uchaguzi Mkuu.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa inasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, NEC, pamoja na kutoa taarifa za uzushi.

"Kitendo cha baadhi ya wagombea wa urais hasa mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu kuikashifu Tume kwamba itaiba kura zake ni kitendo cha kuidhalilisha tume na kutaka kuitisha ili isifanye kazi zake kwa uhuru,’’ alisema Dk. Mahera Charles.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa taarifa kukanusha madai hayo. Bw. Lissu mwenyewe amethibitisha kuwa Jumatatu asubuhi Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini humo ameandikia CHADEMA akitaka chama hicho kueleza kwa nini mgombea wake wa urais anatishia amani.


Barua kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ikipinga uwepo wa kikao chochote cha wasimamizi wa uchaguzi majimbo.




No comments:

Post a Comment