UTAFITI WA KISAYANSI WAONESHA DK.JOHN MAGUFULI ANGESHINDA KWA ASILIMIA 89.5 - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Friday, 25 September 2020

demo-image

UTAFITI WA KISAYANSI WAONESHA DK.JOHN MAGUFULI ANGESHINDA KWA ASILIMIA 89.5

4+%252819%2529
Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

14+%25283%2529Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli.

 Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa Uchaguzi Mkuu ungefayika  Jumatano ya Septemba 23, 2020 tafiti za kisayansi zinaonesha mgombea wake wa Urais Dk. John Pombe Magufuli angeibuka mshindi kwa asilimia 89.5.


Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 25, 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na wanahabari na kutoa tathimini ya kampeni za Chama hicho ambapo amesema kampeni zao zinakwenda vizuri huku wakishambulia kila kona ya nchi yetu.


"Tumekuwa tukifanya tathimini na hali ya mwenendo wa kampeni, uchaguzi mkuu ungekuwa umefanyika Jumatano ya wiki ya Septemba 23, mgombea wetu utafiti wa kisayansi ambao tumeufanya angeshinda kwa asilimia 89.5,"amesema Polepole.


Amesisitiza matokeo ya asilimia hizo ni kwa mujibu wa uchambuzi wa kisayansi."Matokeo haya ni kwa mujibu wa uchambuzi wa kisanyansi kama mnakumbuka tulianza kwa barabara lakini kwa sasa kuna kelkopta ili tufike kila mahali na kufika kwa urahisi."


Ameongeza kuwa helkopta hiyo itatumika katika maeneo mengine lakini asilimia kubwa mgombea wao wa urais atatumia barabara kukutana na wananchi lakini huko mbele ya safari watakuwa na mbinu mpya ya kufanya kampeni zao. Aidha Polepole amesema Mgombea urais wa CCM katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi atashinda kwa kishindo kwani anaendelea na kampeni zake vizuri.


Amefafanua Dkt. Mwinyi ameshafanya mikutano katika Visiwa vya Unguja na Pemba na mwitikio wa wananchi ni mkubwa, hivyo amebaki na deni la kuhakikisha anawaletea maendeleo makubwa kwa kwenda na kasi ya Dk. Magufuli baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.


"Dk. Mwinyi atamshinda yule babu kulee (Maalim Seif) kwa kishindo maana anatafuta kushinda lakini hawezi bali alichonacho ni tamaa ya madaraka ndio inamfanya agombee, wakae tayari kumtia moyo maana ushindi unakwenda CCM tena tutashinda mapema kabisa na kwa kishindo.


"Na yule mzee namwambia asinijaribu mimi maana hana mbio za kukimbizana, hivyo hawezi kushinda na anachoonekana anapenda sana  king’oling’oli, aache kama hataki tutamfundisha adabu,"amesisitiza Polepole.

Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *