MKUU WA WILAYA AKABIDHI CHETI CHA USAJILI WA AMCOS KIMBANGO LUHANGARASI NYASA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 16 September 2020

MKUU WA WILAYA AKABIDHI CHETI CHA USAJILI WA AMCOS KIMBANGO LUHANGARASI NYASA

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba akiwakabidhi Cheti cha Usajili  viongozi wa Kimbango Amkos katikaViwanja vya  Ofisi ya Serikali ya kijiji cha Kimbango kata ya Luhangarasi Wilayani Nyasa. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa bw Jimson Mhagama. Picha na Ofisi ya ded Nyasa.



Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba akiwakabidhi Cheti cha Usajili  viongozi wa Kimbango Amkos katikaViwanja vya  Ofisi ya Serikali ya kijiji cha Kimbango kata ya Luhangarasi Wilayani Nyasa. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa bw Jimson Mhagama. Picha na Ofisi ya ded Nyasa.

Na Netho Credo, Nyasa

MKUU wa Wilaya ya Nyasa Bi. Isabela Chilumba, jana amekabidhi Cheti cha Usajili wa Chama Kipya cha Msingi cha Ushirika wa Mazao Kimbango, ambacho kimesogeza karibu  Huduma ya kuuza mazao kwa wakulima wa Kijiji cha Kimbango kata ya Luhangarasi Wilayani Nyasa, Makabidhiano  yaliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya kijiji  cha Kimbango Wilayani hapa.

Akikabidhi Cheti Cha Usajili amewataka wananchi wa Kijiji hicho, na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla, hususani Vijana, kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa, kwa kuwa Ardhi  ipo ya kutosha inayostawisha zao la kahawa ili kuongeza kipato Ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.

Chilumba alifafanua kuwa,  wananchi wa kijiji cha Kimbango wamefurahia kupewa Cheti cha Usajili wa Chama Cha Ushirika cha Msingi, ambacho ilikuwa ni  kero ya wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa, awali walikuwa wanasafirisha mazao yao umbali mrefu, na walikuwa wakiuza Kwenye Chama cha Luhangarasi Amcos, lakini kwa sasa watakuwa wanauza katika Chama chao ambacho kimepata usajili.

Aliongeza kuwa, wasifurahie kupata usajili tu peke yake bali waongeze uzalishaji wa zao hilo, kwa kuongeza mashamba mapya na kupanda mbegu bora za kisasa, ambazo huzalisha mazao mengi na kwa muda mfupi. Badala ya kusubiri mashamba ya kurithi peke yake. Amewaagiza Watendaji wa Kata na Kijiji kuhakikisha kila mkulima anaongeza Uzalishaji wa zao la Kahawa kwa kila Msimu wa kilimo.

“Ndugu wakulima nimewaona leo mnafurahia kupewa cheti cha Usajili wa Chama chenu, lakini furaha hiyo isiishie hapa bali iwe fursa kwenu ya kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa hapa kijini kwenu na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla, hasa vijana kila kijana anatakiwa kuwa na walao hekari mbili kwa kufanya hivi hata chama chenu cha ushirika kitakuwa na nguvu kwa kuwa kitakuwa na mazao mengi”.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuwa waaminifu na waadilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kulinda na kutunza Fedha na mali ya Chama ili wananchi wakipende Chama chao, na kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Pia aliwatahadharisha kuwa Serikali Wilayani hapa ipo makini na itawachukulia hatua za kisheria Viongozi wa Vyama vya Ushirika watakaohusika na Wizi au upotevu wa Fedha za wakulima.

Kwa upande wao wanachama na wakulima wa mazao Katika Kijiji hicho wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuwawezesha wakulima kuuza mazao yao katika Vyama vya Ushirika ambavyo vinawakomboa kiuchumi na kuwaunganisha na huduma za kibenki kwa kuwa awali walikuwa hata benki hawakujui.Aidha wamemwambia Mkuu wa Wilaya kuwa wataongeza uzalishaji wa zao la kahawa ili waweze kuongeza uchumi wa kaya na Taifa kwa ujumla wake.


No comments:

Post a Comment