WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao hicho kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa na wa pili kulia ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini kuzingatia uwazi na uwajibikaji kwenye shughuli zao ikiwemo fedha hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Ummy ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa asasi za kiraia (NGOs) zinazofanya kazi Halmashauri ya Jiji la Tanga na mkoa wa Tanga ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali
Alisema hategemei kuona shirika lisilokuwa la kiserikali linapata fedha za kwa ajili ya kuchochea mpasuko na masuala yatakayoleta mfarakano kati ya watanzania kubwa waendelee kuheshimu sheria, kanuni zinazosimamia mashirika hayo.
Aidha alisema lazima wafanye kazi kwa malengo waliyoyaomba na sio kujiingiza kwenye masuala mengine yatakayohatarisha umoja na mshikamano kwenye nchi ambayo ni tunu kubwa.
Waziri Ummy aliyataka pia mashirika hayo kuhakikisha rasilimali fedha wanazozipata ambazo wanaziomba kwa jina la watanzania kuzitumia kikamilifu kwa ajili ya wananachi wanaoombea fedha hizozna sio kwa maslahi yao binafsi.
“Lakini kubwa amesisitiza uwazi na uwajibukaji kwa asasi za kiraia kwa wananchi na serikali na ndio maana mwaka 2019 tulitoa kanuni mpya za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanazitaka kila asasi inayopokea fedha inayozidi milioni 20 kuhakikisha inatoa taarifa kila baada ya miwezi mitatu kwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii namna zitakavyotumika na matokeo yanayotarajiwa”Alisema
Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira amewaambia viongozi wa asasi hizo mkoani Tanga huku akieleza kazi yake kubwa ni kuwa kiunganishi kati ya NGOs, Bunge, Serikali, CCM na wafadhili ili waweze kupata mafanikio.
Alisema dhamira ya kukutana na viongozi wa NGOs za Mkoa wa Tanga ni dhumuni kubwa likiwa ni kumwezesha kupata uelewa wa changamoto zao ili aweze kuandaa vipaumbele vyake.
Alisema kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi hizo hapa nchini na ndio maana katika vipaumbele vikuu vya CCM kwenye ilani ya mwaka 2025
Neema aliwathibitishia viongozi wa (NGOs) mkoa wa Tanga kwamba CCM inatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi hizo nchini na ndio maana katika vipaumbele vyake vikuu kwenye ilani a 2020 -2025
“Kuchukua hatua madhubuti za kujenga mazingira wenzeshi kwa asasi za kiraia, kidini na vyombo vya habari kulinda kustawi ili kuchangia maendeleo ya Taifa”Alisema Neema.
Aidha alisema maendeleo hayana chama wala dini hivyo kupitia nafasi hiyo atahakikisha anawaunganisha ili kuweza kuwa chachu kubwa ya maendeleo kwao.
“Lakini wana Tanga mtambue kwamba nyie ni asasi za kwanza za kiraia ambao tunakutana nanyi tokea nimetangazwa Agosti 20 mwaka huu naamini wadau wa asasi za kiraia hatuna mambo ya vyama
“Ila mtanisamehe siku ya leo wakati narejea ilani ya CCM muone namna gani ilani inatambua NGOs kama wadau muhimu ambao wanashirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii yetu”Alisema
No comments:
Post a Comment