WANANCHI WA MKOA WA SIMIYU WATEMBELEA MABANDA TAASISI ZA SEKTA YA UCHUKUZI MKOANI SIMIYU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 5 August 2020

WANANCHI WA MKOA WA SIMIYU WATEMBELEA MABANDA TAASISI ZA SEKTA YA UCHUKUZI MKOANI SIMIYU



Afisa Uhusiano wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Bi. Amina Uddi, akimwelekeza mwananchi namna ya kuvaa boya, wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Bi. Ruth Kigera, akigawa kipeperushi kwa  mwananchi wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.



Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya VIwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mariam lusewa, akiwaonesha wananchi viwanja ambavyo vinatumika kusafirishia mazao, wakati wananchi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.



Mwananchi ambaye hakutaja jina lake, akifafanua jambo kwa Meneja wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mkoani Mwanza, Bw. Hamid Mwikombe (aliyekaa), wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Asha Mwikombe.


Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Bi. Mecklina Merchades, akiwaeleza wakazi wa Simiyu namna wanavyosoma viwango vya joto wakati wa usomaji wa hali ya hewa, wakati wakazi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment