WADAU SEKTA YA UTALIIWAZOA TUZO ZA TANAPA ZA UTALII MWAKA JIJINI ARUSHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 7 August 2020

WADAU SEKTA YA UTALIIWAZOA TUZO ZA TANAPA ZA UTALII MWAKA JIJINI ARUSHA

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Kamishina Mkuu wa Uhifadhi wa TANAPA Dkt. Allan Kijazi akizungumza na wadau wa sekta ya Utalii leo jijini Arusha wakati wa hafla fupi ya utoaji wa Tuzo za Utalii za TANAPA 2020 jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Aloyce K. Nzuki akielezea faida ya Tuzo za TANAPA za utalii kwa wadau waliohudhuria tuzo za TANAPA za Utalii kwa Mwaka 2020, zilizofanyika mapema leo Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akizungumza na wadau wa sekta ya Utalii wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Utalii za TANAPA kwa mwaka 2020 leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa tuzo za utalii za TANAPA 2020 kwa mwakilishi wa kampuni ya Leopard Tour E. Kimario jijini Arusha leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa Tuzo ya utoaji huduma Bora za Utalii ya TANAPA 2020 kwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Kampuni ya Zara Tours, Zainab Ansell leo jijini Arusha. Wengine wanaoshuhudia Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi.4

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa Tuzo ya utoaji huduma za Utalii ya TANAPA 2020 kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ahsante Tours, Cuthbert Swai leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa tuzo za TANAPA 2020 kwa watoa huduma  za utalii Bora kwa mwaka 2020 jijini Arusha leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa shughuli za Utalii Tanzania ( TATO), Willy Chamburo akifurahia Tuzo ya Utalii ya TANAPA wakati akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla leo jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment