Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali leo kwa kushirikiana na kampuni ya uuzwaji wa simu za mkononi,Infinix, wamezindua Infinix hot 9 play.
Kupitia kauli mbiu ya Maonesho kwa Mwaka 2020 isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020“. Tigo imeweza kumsaidia mkulima kutatua changamoto mbali mbali Tanzania nzima.
Akizungumza leo jijini Dodoma Meneja wa bidhaa za intaneti kutoka Tigo Mkumbo Myonga amesema katika maonesho hayo wameingia makubaliano na baadhi ya kampuni za uuzaji vifaa vya simu ambazo zina sifa na ubora kwa matumizi ya watanzania.
Kwa upande wa Infinix Meneja Uhusiano,Saiphon Asajile, amesema kwamba simu hii ya Hot 9 play, ni simu janja inayokaa na chaji kwa muda mrefu, simu hii inauzwa Tshs 320,000, na mteja atakapo nunua atapata intaneti 78 GB bure kwa mwaka mzima na waranti miezi 13.
Msimu huu wa Nane nane, kuwa mmiliki wa simu janja kutoka Tigo kwa bei nafuu,na upate intaneti 78GB bure kwa muda wa mwaka mzima,kwaajili ya kuperezi na kufurahia mtandao wenye kasi wa Tigo 4G+.
Tembelea mabanda ya Tigo katika viwanja vya Nane Nane
· Morogoro· Dodoma· Simiyu· Arusha Mwanza· Tabora· Mbeya· Lindi
Miliki simu janja leo ili uweze kufurahia huduma na bidhaa kama Tigo Pesa na vifurushi vya intaneti na pia kuisajili laini yako ya simu kwa mfumo wa alama za vidole. Tigo Live it,Tigo love it.
No comments:
Post a Comment