MTANDAO WA ELIMU TANZANIA WAWAZAWADIA WAZAZI NA WANAFUNZI WA MFANO, KATA YA MRIJO CHEMBA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 21 August 2020

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA WAWAZAWADIA WAZAZI NA WANAFUNZI WA MFANO, KATA YA MRIJO CHEMBA

Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Bw. Ochola Wayoga akitoa zawadi kwa mmoja wa wazazi Kata ya Mrijo, wilayani Chemba aliyejitolea katika ushiriki wa utatuzi kero za elimu eneo lake kwenye hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kata ya Mrijo. Katika hafla hiyo wnachama wa TENMET walitoa mifuko 50 ya simenti kuchangia kukamilika kwa bweni la wanafunzi sekondari ya Mrijo lililoanza kujengwa na Serikali kwa kushirikiana na wazazi.


Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (kushoto) akitoa zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kata ya Mrijo aliyefanya vizuri katika masomo yake, kwenye hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kata ya Mrijo.


Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi aliyefanya vizuri katika masomo yake, kwenye hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba. Kushoto ni Afisa Rasilimali, TENMET, Seif Hassan akiratibu mchakato huo.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari Kata ya Mrijo, wilayani Chemba wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu, eneo hilo ambapo shughuli mbalimbali za kuhamasisha elimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii nyingine zilifanyika, sambamba na utoaji zawadi.

Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) pamoja na wanachama wa utandao huo wakitembelea shule ya sekondari Mrijo kuangalia Bweni lililojengwa na Serikali kushirikiana na wananchi walojitolea ikiwa ni jitihada za kutatua kero anuai za elimu eneo, Kata ya Mrijo. TENMET imetoa mifuko 50 ya simenti kuchangia kukamilika kwa bweni hilo ili liweze kusaidia wanafunzi eneo hilo.

Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza jambo na wanachama wa TENMET walipotembelea shule ya sekondari Mrijo kuangalia bweni lililojengwa na Serikali kushirikiana na wananchi walojitolea ikiwa ni jitihada za kutatua kero anuai za elimu eneo, Kata ya Mrijo.


Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza jambo na wanachama wa TENMET walipotembelea shule ya sekondari Mrijo kuangalia bweni lililojengwa na Serikali kushirikiana na wananchi walojitolea ikiwa ni jitihada za kutatua kero anuai za elimu eneo, Kata ya Mrijo.


Mwalimu Mkuu, Sekondari ya Mrijo, Hance Mwaitete (wa pili kulia) akiwaongoza wadau wa TENMET na maofisa elimu kutoka wilaya ya Chemba kutembelea shule hiyo. Mtandao wa Elimu ulitoa mifuko 50 ya simenti kuchangia kukamilika kwa bweni la wanafunzi shuleni hapo ili iiweze kusaidia wanafunzi.


Mwalimu Mkuu, Sekondari ya Mrijo, Hance Mwaitete (katikati) akiwaongoza wadau wa TENMET na maofisa elimu kutoka wilaya ya Chemba kutembelea shule hiyo. Mtandao wa Elimu ulitoa mifuko 50 ya simenti kuchangia kukamilika kwa bweni la wanafunzi shuleni hapo ili iiweze kusaidia wanafunzi.


Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari Kata ya Mrijo, wilayani Chemba wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu, eneo hilo ambapo shughuli mbalimbali za kuhamasisha elimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii nyingine zilifanyika, sambamba na utoaji zawadi.


Mwalimu Mkuu, Sekondari ya Mrijo, Hance Mwaitete akizungumza na wadau wa TENMET, wazazi na wanafunzi kwenye hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kata ya Mrijo, ambapo shughuli mbalimbali za kuhamasisha elimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla zilifanyika, sambamba na utoaji zawadi.

Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga akizungumza na wazazi na wanafunzi kwenye hafla ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kata ya Mrijo, ambapo shughuli mbalimbali za kuhamasisha elimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla zilifanyika, sambamba na utoaji zawadi.


Afisa Rasilimali wa TENMET, Seif Hassan akiendesha mjadala wa elimu na wazazi wa Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu eneo hilo.


Mijadala wa elimu na baadhi ya walimu Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba ikiendelea katika Juma la Elimu eneo hilo.


Afisa Habari wa Uwezo Tanzania, Greyson Mgoi akiendesha mjadala wa elimu na wazazi wa Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu eneo hilo.


mijadala wa elimu na wanafunzi Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba ikiendelea ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu eneo hilo.


No comments:

Post a Comment