Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole. |
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewataka wanachama ambao hawakuteuliwa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya chama hicho uliokamilika jana.
Bw. Humphrey Polepole amesema hayo leo katika maojiano na Kituo cha Channel 10 jijini Dodoma, kuzungumzia mchakato na namna chama hicho imejipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika hapo Oktoba, 2020. Kiongozi huyo amefafanu kuwa wanachama waliokosa uteuzi hawana budi kuwa watulivu na kukubaliana na maamuzi ya ngazi za uteuzi waliojiwekea ili kuendelea kukijenga chama.
Amebainisha mchakato huu wa chama ni sehemu ya awali ya kujenga timu ya utendaji mara baada ya uchaguzi kumalizika, kwani baada ya uchaguzi CCM ikishinda Serikali itakayoundwa inaitaji timu ya watendaji ambao wanaweza kuwa wao au yeyote mwenye sifa. Amesema CCM ni taasisi kubwa yenye wanachama wengi kuliko vyama vingine hivyo lazima chama hicho kifuate demokrasia, kanuni na taratibu za chama kupata viongozi wake.
Aliwaomba waliokosa nafasi kwa sasa kuungana na kuendelea kufanya kampeni na walioteuliwa ili chama kipate ushindi wa kishindo na kuendelea kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo makubwa.
Akizungumzia maandalizi ya kampeni ya chama hicho alisema, CCM imejipanga vizuri na itafanya mambo makubwa na ya kihistoria kwenye kampeni zinazokuja.
"...Tunakwenda kupeleka maudhui ya chama kwa wanachama wetu na Watanzania, tutafanya kampeni kistarabu na kisayansi kwa hali ya juu. Wasanii wote wa sanaa na burudani wote wako ndani ya Chama cha Mapinduzi, kuna wasanii takribani 270 wameimba nyimbo kutangaza mambo mbalimbali mazuri yaliofanywa na Serikali yetu na pia kuna zaidi ya nyimbo 700 zimeimbwa. Tuna timu nzito ya kampeni...hivyo ushindi kwetu ni uhakika na wananchi wategemee makubwa," alisisitiza Bw. Polepole.
No comments:
Post a Comment