WANANCHI WAMZAWADIA RAIS MAGUFULI BONGE LA JOGOO AKIZUNGUMZA NAO NANGULUKULU, SOMANGA AKITOKEA MSIBANI MTWARA - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP

Habari Mpya

.com/img/a/

Thursday, 30 July 2020

demo-image

WANANCHI WAMZAWADIA RAIS MAGUFULI BONGE LA JOGOO AKIZUNGUMZA NAO NANGULUKULU, SOMANGA AKITOKEA MSIBANI MTWARA

5+%252829%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jogoo alilopewa na Mzee Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge.

9+%252811%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Somanga mkoani Lindi mara baada ya kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara. PICHA NA IKULU.

1..+%25282%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi- Somanga wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mwara leo tarehe 30 Julai 2020.


2+%252863%2529
Wananchi wa Nangulukulu wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao wakati akitokea Masasi leo.

8+%252812%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo.

11+%25289%2529
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Nangulukulu-hadi Somanga mkoani Lindi ambapo sehemu ya barabara yake imeharibika vibaya na kuhitaji matengenezo makubwa .

Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *