JPM AIINGIZA TANZANIA KATIKA UCHUMI WA KIPATO CHA KATI, BENKI YA DUNIA YATHIBITISHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 2 July 2020

JPM AIINGIZA TANZANIA KATIKA UCHUMI WA KIPATO CHA KATI, BENKI YA DUNIA YATHIBITISHA

Mradi Mkubwa wa kufua umeme kwa maji nchini Tanzania, Julius Nyerere (MW 2115).

BENKI ya Dunia imeiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati.

Hatua hii inajiri miaka mitano kabla ya mipango ya maendeleo ya taifa hilo ambapo ilikuwa imelenga kuafikia kiwango hicho kufikia 2025. Na kufuatia hatua hiyo Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewapongeza wananchi wa taifa hilo kwa mafanikio hayo.

Kulingana na mchanganguzi wa masuala ya kiuchumi kutoka Tanzania Deus Kibamba benki hiyo hutazama pato la taifa kwa mfano kupitia jumla ya utajiri wa raslimali na ule wa kifedha na kugawanya na idadi ya watu wa Tanzania.

Amesema kwamba mataifa yenye kipato cha kati ya dola 1,006 hadi dola 3,955 kwa mtu mmoja hutajwa kuwa mataifa yenye kipato cha kati, lakini yaliyo na uchumi mdogo huku yale yenye kipato cha kati ya dola 3,956 hadi dola 12,235 yakidaiwa kuwa mataifa yenye kipato cha kati yenye uchumi unaoimarika.

Kulingana na mchanganguzi wa masuala ya kiuchumi kutoka Tanzania Deus Kibamba, ni kwamba taifa hilo linaelekea kuimarika kiuchumi.

Kibamba anasema ni ishara kwamba siasa za taifa hilo zinaenda sambamba na ukuaji wa chumi wa taifa hilo na kwamba sifa hiyo italisaidia taifa hilo kuvutia uwekezaji zaidi wa kigeni hatua ambayo italifanya kuimarika zaidi kiuchumi.

Hatahivyo amesema kwamba Watanzania hawapaswi kufikiria kwamba mifuko yao tayari itaanza kufaidiki kutokana na hilo, na badala yake akasema wanahitajika kufanya bidii zaidi ili kuboresha uchumi.

Kulingana na Kibamba hatua ya uongozi uliopo kudhibiti matumizi ya fedha mbali na kukabiliana na uvujaji wa fedha ni miongoni mwa hatua muhimu zilizochukuliwa na serikali kufikia malengo hayo yaliotarajiwa mwaka 2025.

Kulingana na benki ya dunia mataifa yenye kipato cha kati ndio yenye asilimia 75 ya idadi ya watu mbali na asilimia 62 ya watu masikini duniani.
-BBC

No comments:

Post a Comment