Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akihutubia wakati akizindua Mradi wa Lishe Imara mkoani hapa jana unaoendeshwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Action Against Hunger. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Victolina Rudovick.
Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi, akizungumzia umuhimu wa lishe kwenye uzinduzi huo.
Mratibu wa mradi huo, Daud Tano akizungumzia lengo la mradi huo utakaofanyika katika mikoa ya Singida na Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Victolina Rudovick, akizungumza.
Afisa Lishe Mwandamizi Taasisi ya Chakula na Lishe, Maria Msangi akizungumza. Kulia ni Mratibu wa mradi huo, Daud Tano.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akizungumza.
Mratibu wa Mradi wa USAID Boresha Afya (Egpaf) Mkoa wa Singida, Dk.Nicholaus Njoka, akizungumza.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi, akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Action Against Hunger.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ameliomba Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Action Against Hunger kuanzisha kituo cha kutoa tiba kwa watu wenye utapiamlo mkoani hapa.
Dk. Nchimbi alitoa ombi hilo jana wakati akizindua Mradi wa Lishe Imara mkoani hapa unaoendeshwa na shirika hilo mkoani Dodoma na sasa Singida.
Alisema suala la Lishe halihitaji mgongano wa kifikra,ni suala lililonyooka halina ama halina au ni mwelekeo mmoja tu na ni kweli na ni yakini.
"Nasema hivyo ili kuonyesha kwamba mradi huu ni wa umuhimu sana kwa jamii na ninapendekeza kituo hicho cha kutoa tiba kwa watu wenye utapiamlo kijengwe hapa Singida." alisema Dk. Nchimbi.
Dk. Nchimbi alisema kuna kila sababu ya kituo hicho kujengwa Singida kwa kuwa kitakuwa jirani ya makao makuu ya nchi na kwamba eneo la kujenga kituo hicho lipo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kubwa ya kanda.
Akizungumzia mradi huo Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi alisema mradi huo wa Lishe Imara kwa Mkoa wa Singida unafaida kubwa,utawahusu wamama wajawazito,wamama wanaonyonyesha na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
"Makundi hayo mkuu wa mkoa umekuwa ukielekeza mara kwa mara kuhakikisha tunapunguza vifo pamoja na mambo mengine hivyo ni lazima suala la lishe likae sawa sawa na mama hatakuwa na changamoto yoyote ya kiafya na atajifungua salama" alisema Lutambi.
Mratibu wa Mradi huo Daud Tano alisema utalenga kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika Mkoa wa Singida na Dodoma.
Alisema Mradi wa Lishe Imara unalengo Mahususi kutujengea Hospitali,Vituo vya Afya pamoja na Zahanati jinsi ya kutambua, kutibu na kutoa huduma stahiki ya masuala ya utapiamlo.
Alisema shabaha nyingine ya mradi huo ni kupunguza hali ya udumavu kwa watoto wa miezi 0-59 kutoka asilimia 34 kwa 2015 hadi asilimia 28 ifikapo 2021 na kuzuia maambukizi mapya ya Utapiamlo mkali kwa watoto wa miezi 0-59 kwa asilimia 5 ifikapo 2021. Na kuongeza idadi ya watoto wenye umri wa miezi 0-5 wanaonyonya maziwa ya mama pekee kutoka asilimia 41
(TNNS 2014) hadi kufikia asilimia 50 ifikapo 2021.
Tano alisema Mradi huo watautekeleza katika Halmashauri nne ambazo ni Mpwapwa,Itigi,Mkalama pamoja na Iramba.
Mradi huo unalenga kuwafikia Vijana na watoto walio chini ya umri wa Miaka mitano na huduma zinazohusiana na Lishe hii ni pamoja na upimaji,matibabu pamoja na kuwajengea uwezo watoa huduma katika jamii.
No comments:
Post a Comment