MWAKA WA FEDHA WA 2020/ 2021 WIZARA YA MAJI KUFANYA USANIFU WA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 22 June 2020

MWAKA WA FEDHA WA 2020/ 2021 WIZARA YA MAJI KUFANYA USANIFU WA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA DODOMA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo akizungumza mkoani Singida, mwishoni mwa wiki kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya mikoa hiyo.

 Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo, akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Mhandisi Lucas Saidi, akizungumza.

Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza mabomba cha Pipe Industries Company Ltd, Ezra Chiwelesa, akizungumza.


Mabomba yaliyokabidhiwa.

Mabomba yakiwa kwenye gari.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo akizungumza na Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo.


Na Mwandishi Wetu, Singida

WIZARA ya Maji inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka ziwa vicktoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17,Singida ikiwa ni moja ya mikoa hiyo.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa maji alisisitiza kwamba kwa kuwa fedha za mradi huo zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha,hivyo anaamini katika kipindi cha miaka mitano ijayo mikoa ya Singida na Dodoma inaweza ikapata maji kutoka ziwa Viktoria.

“Na utafiti wa awali umeonyesha kwamba jambo hili linawezekana  wameshaona wataalamu wetu kwamba maji ya kifika pale Meatu wataweza wakayapandisha yakafika katika Kijiji cha Kisana,katika Mji mdogo wa Kiomboi.”alifafanua Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maji.

Hata hivyo Prof. Mkumbo aliitaja mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mara pamoja na Simiyu kuwa ni mikoa ambayo kiraslimali ya maji nimikoa kame na ndiyo yenye changamoto ya kupata mvua kidogo na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa maji.

“Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mara pamoja na Simiyu hii ni mikoa ambayo kiras;imali za maji ni tunasema ni mikoa ambayo ni mikoa kame inachangamoto za kupata mvua kidogo kwa hivyo maji ni kidogo sana na kwa kiasi kikubwa tunategemea maji chini ya ardhi.”aliweka bayana Prof Mkumbo.

Hata hivyo Prof Mkumbo alisisitiza pia kwamba kwa bahati nzuri kwa mikoa ya Tabora,Shinyanga,Simiyu pamoja na Mara wamekwishatatua changamoto zilizokuwa zikiikabili mikoa hiyo kwa kutumia raslimali kubwa ya Ziwa Viktoria.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa wizara maji ya ziwa viktoria wameyafikisha mpaka wilayani Igunga,Mkoani Tabora yameshakamilika na wananchi wa Igunga tayari wanapata maji kutoka ziwa viktoria.

Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo aliweka wazi kwamba kupitia mabadiliko ya kisera ndani ya sekta ya maji hivi sasa wachimbaji wa visima ni sehemu ya RUWASA,ambapo ni kitengo kilicho ndani ya Mamlaka hiyo.

“Kwa hiyo tutataka tupihe kambi katika Mkoa wa Singida kuhakikisha kwamba tunatafuta vyanzo na tunatekeleza miradi kadri inavayowezekana ili wastani wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Singida uweze kupanada angalau uweze kufikia kama mikoa mingine.”alifafanua Mkurugenzi huyo wa RUWASA.

Aidha Kivegalo hata hivyo aliweka bayana kuwa alitumia fursa hiyo kuwaagaiza mameneja wengine wa RUWASA wa mikoa yote kukimbizana na kasi kama meneja wa Mkoa wa Singida alivyofanya ambapo takribni miradi yote imeshafikia asilimia sabini.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Mhandisi Lucas Saidi alifafanua kwamba kuna miradi zaidi ya 30 inayotarajiwa kutekelezwa lakini kutokana na mabomba hayo yaliyopo wanatarajia kutekeleza jumla ya miradi tisa iliyopo katika wilaya za Mkoa wa Singida.

Mhandisi huyo wa RUWASA hata hivyo aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa Wembere na Kyalosangi wilayanai Iramba, mradi wa Ibaga wilayani Mkalama,mradi wa Mughamo na Msisi wilaya ya Singida, mradid wa Dung’unyi wilayani Ikungi na mradi wa Kitaraka, Kikombo na Kashangu wilayani Manyoni.

Kwa mujibu wa Mhandisi Swedi jumla ya watu 63000 wanatarajia kunufaiaka na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na kwamba zaidi ya miradi 40 inatarajiwa kukamilika katika kipindi hicho.    

No comments:

Post a Comment