MENEJIMENTI SEKTA YA UCHUKUZI YARIDHISHWA NA UJENZI MELI MPYA, CHELEZO NA UKARABATI WA MV. VIKTORIA NA MV. BUTIAMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 24 June 2020

MENEJIMENTI SEKTA YA UCHUKUZI YARIDHISHWA NA UJENZI MELI MPYA, CHELEZO NA UKARABATI WA MV. VIKTORIA NA MV. BUTIAMA

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya sehemu ya chini ya meli Mpya ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” inayojengwa katika bandari ya Mwanza Kusini, jijini Mwanza. Ujenzi wa Meli hiyo unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2021 na itagharamu zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 80.

Mafundi wa Kampuni ya GAS EntecCo Ltd, Kang Nam Cooperation ya Korea Kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania inayojenga meli ya MV Mwanza, wakiendelea na kazi ya ujenzi wa meli hiyo, inayojengwa jijini Mwanza.

Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL), Luteni Kanali Mhandisi Abel Gwanafyo akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa Kazi Tu”, Ukarabati wa meli ya MV Butiama, MV Viktoria na Ujenzi wa Chelezo, mkoani Mwanza.

Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL), Luteni Kanali Mhandisi Abel Gwanafyo akiwaonesha wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo, mabadiliko yaliyofanywa kwenye mifumo ya uendeshaji wa meli ya MV Viktoria wakati walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa Kazi Tu”, Ukarabati wa meli ya MV Butiama na MV Viktoria na Ujenzi wa Chelezo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lucas Kambeleje.

No comments:

Post a Comment