WANANCHI SINGIDA WALIPONGEZA SHIRIKA LA SEMA KWA UTOAJI ELIMU YA KUJIKINGA VIRUSI VYA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 12 May 2020

WANANCHI SINGIDA WALIPONGEZA SHIRIKA LA SEMA KWA UTOAJI ELIMU YA KUJIKINGA VIRUSI VYA CORONA

Maafisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Mary Kilimba  (kushoto) na Veronica Peter wakitoa elimu kwa wananchi kwa njia ya mabango katika Barabara ya Arusha mjini hapa leo namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Ipyana Mwakyusa akitoa elimu hiyo kwa dereva wa Bajaji.
Daria  John na Geryson Janga wakitoa elimu hiyo kwa njia ya mabango.

Geryson Janga akitoa elimu hiyo kwa njia ya mabango.

Mkazi wa Kata ya Mitunduruni, Rahama  Moshi (kushoto) akizungumza na maafisa wa Shirika la SEMA.

Maafisa wa Shirika la SEMA, wakitoa elimu kwa dereva Bodaboda. Kushoto ni Afisa Mradi wa SEMA, Renard Mwasambili na Daria  John.

Ipyana Mwakyusa akitoa elimu hiyo kwa wananchi.

Amani Twaha,  akitoa elimu.

Elimu ikitolewa kwa wasafisha viatu.

Witness  Anderson, akitoa elimu kwa muuza  mitumba.

Ipyana Mwakyusa akitoa elimu hiyo kwa madereva wa bajaj.

Mary Kilimba  (kulia) na Veronica Peter wakitoa elimu hiyo kwa njia ya mabango.

Wananchi wakiwa wamevaa barakoa kujikinga na Corona.

Tatu Muna, akizungumzia kuhusu Corona.


Na Dotto Mwaibale, Singida.

WANANCHI mkoani Singida wamelipongeza  Shirika lisilokuwa la Serikali Sustanable Environment Management Action (SEMA) kwa utoaji elimu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Covid 19 vinavyo sababisha Ugonjwa wa Corona.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wananchi hao akiwemo Tatu Muna amepongeza hatua hiyo kwani itasaidia kuwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Nalipongeza Shirika hili kwa hatua hii waliyoichukua ya kutoa elimu ya kujikinga na Corona lakini ombi langu kwa Serikali watoe idadi ya watu wanaoumwa ugonjwa huo jambo litakalosaidia wananchi kuchukua tahadhari kubwa."alisema Muna.

Mkazi wa Mitunduruni Rahama Moshi alisema kuwa pamoja na elimu hiyo kutolewa maeneo ya mjini ni vizuri pia kama itapelekwa maeneo ya vijijini ambako watu wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huu.


Akielezea kuhusu utoaji wa elimu hiyo Ofisa kutoka Shirika la SEMA Ipyana Mwakyusa alisema homa kali ya mapafu inayosababisha Virusi vya Corona ni Ugonjwa unaoambukizwa kwa kuingiawa na maji maji yatokayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye Ugonjwa huo anapokohoa ama kupiga chafya.


Alieleza jinsi ya kujikinga na Ugonjwa huo alitoa tahadhari ya watu kukaa mbali angalau mita moja au mbili jambo litakalosaidia kujiepusha na maambukizi iwapo mmoja kati ya watu hao atakuwa na maambukizi.

Mwakyusa alitaja tahadhari nyingine inayopaswa kuchukuliwa ni kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono,kuepuka kugusana na mtu mwenye dalili za Ugonjwa huo,kusalimiana kwa kushikana mikono,kukumbatia na kubusiana.

"Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka kwa kutumia sabuni au dawa ya kutakasa mikono na baada ya kunawa epuka kugusa macho,pua au mdomo na nguo badala yake jifute kwa kutumia tishu ambayo itatupwa sehemu salama baada ya kutumika."alisema Mwakyusa.

Afisa mradi kutoka SEMA Renard Mwasambili alisema utoaji wa elimu hiyo umekuwa na mafanikio kwani mwitikio wa wananchi umekuwa ni mkubwa na kuongeza kuwa kwa siku ya leo wametoa elimu hiyo kwenye maeneo ya mitaa ya Unyankindi,Mwenge,Utemini na maeneo ya Hospitali ya Mkoa.

No comments:

Post a Comment