Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kusaidia mapambano ya virusi vya Covid 19 kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Jeshi la Polisi Mkoa huo kutoka kwa Mtendaji Mkazi wa Kiwanda cha Tanga Saruji cha Cement PLC Mhandisi Benedict Lema kushoto wanaoshuhudia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari kulia na kushoto Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kusaidia mapambano ya virusi vya Covid 19 kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Jeshi la Polisi Mkoa huo kutoka kwa Mtendaji Mkazi wa Kiwanda cha Tanga Saruji cha Cement PLC Mhandisi Benedict Lema kushoto wanaoshuhudia ni kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari.
KIWANDA cha Kuzalisha Saruji cha Tanga Cement (PLC) wamekabidhi msaada wa vifaa vya kinga kwa ajili ya kusaidia mapambano ya virusi vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID 19) kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Jeshi la Polisi Mkoani hapa ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali kukabiliana nao.
Makabidhiano ya msaada huo umefanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo Mtendaji Mkazi wa Tanga Cement PLC, Mhandisi Benedict Lema alimkabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella huku akihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Judica Omari na Kamanda wa Polisi mkoa Blausis Chatanda.
Msaada ambao ulitolewa kwa hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ni Apron 200, vipima joto (Infrared) 5, Barakoa (N95) 200, Vipukusi (Sanitezer) lita 100 na Mashine za kuhifadhia Tissue 30 huku kwa upande wa Jeshi la Polisi mkoa nao wakikabidhiwa Barakoa (N95) 200, vipima joto (Infrared) 10 na sabuni ya maji lita 100 huku wakihaidia kutoa mashine za kutolea vipukusi 50 kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa huo.
Akizungumza wakati mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema kwamba wanaishukuru Tanga Cement kwa namna walivyoguswa na kuwaunga mkono kushirikiana nao kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona kama mnavyofahama nchi ipo kwenye Ugonjwa.
Alisema kwamba kama serikali ilikuwa imefanya maandalizi ya kukabiliana na magonjwa aina yote lakini yapo mengine wadau wanahitajika kushirikia na serikali kuweza kuona namna ya kupambana nayo kuhakikisha yanakwisha hivyo msaada huo umefika wakati muafaka.
“Tunaishukuru Tanga Cement kutusaidia vifaa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na Jeshi la Polisi ambao wanafanya kazi kubwa na niwahakikishie msaada mlioutoa umekuja wakati muafa na Ras yupo hapa atahakikisha vinafika kwenye maeneo yaliyokusudiwa,”alisema RC Shigella.
“Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli ameeleza watu wachape kazi hivyo tunashukuru Tanga Cement kwenye kipindi cha Ugonjwa hawajatetereka na wana soko la uhakika na wameendelea kufanya vizuri niwaombe wenye viwanda na wazalishaji wengine wazalishaji ikiwemo,mifugo,uvuvi,misitu na viwandani kilimo wasitetereke kwa sababu ya Corona waende wakazalisha”Alisema
Alisema kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kujiimarisha na kujitegemee kwenye Taifa letu huku akionyesha kufarijika na kuarifiwa kwamba vifaa hivyo vimenunuliwa hapa nchini hivyo vitakuwa vina viwango vya ubora ambao unahitajika.
Awali akizungumza wakati makabidhiano hayo Mtendaji Mkazi wa Kiwanda hicho Mhandisi Benedict Lema alisema wao waliguswa sana kwani jambo hilo ni vita ya ulimwengu na nchi yetu ipo kwenye ulimwengu huu kama ilivyo Jemadari Rais wa nchi Dkt Magufuli anavyosema lazima tusaidiena naye kupambana na janga hilo.
“Leo tumefika kutoa msaada huo ambao unakaribia milioni 20 ikiwemo kufanya patisheni katika hospitali ya Mkoa ya Bombo na eneo la kupumzikia ili watu wawe mbalimbali vilevile tumeleta vifaa vya kujikinga na tumelenga makundi mawili Hospitali na Jeshi la Polisi kwa sababu wao ndio wanapeleka oda na kwenye ugonjwa huo polisi wapo mstari wa mbele”Alisema Mhandisi Lema
Hata hivyo alisema kama rais alivyosema watu wachape kazi ni kweli wameendelea kuchapa kazi na hawajafunga kiwanda wameendelea na uzalishaji na wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa wafanyakazi na watu wanaotembelea kiwanda hicho kwa kupimwa kabla ya kuingia kuendelea na shughuli.
“Ombi langu kwa wadau wengine kwenye mkoa huu na sehemu nyengine zozote zishiriki katika kumuunga mkono Rais na mkuu wa mkoa wananchi wetu waweze kuwa salama “Alisema Mhandisi Lema.
Naye kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari alisema msaada huo utawasaidia kuimarisha juhudi zao za kujikinga na janga la kitaifa la Ugonjwa wa Corona itasaidia kwani bajeti ambayo wanaisimamia ilikuwa haijaweza kubebe vitu vikubwa kama hivyo ambavyo ni janga la ulimwengu mzima.
Alisema kwamba msaada huo utakuwa ni chachu kubwa kwao na utakwenda kujaziliza mapengo yaliyopo na kuweza kuimarisha hususani watumishi idara ya afya kwa kusaidia kujipima na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wanafika kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment