DC AMPA SIKU 7 MHANDISI WA JIJI LA ARUSHA KUWEKA MAJI KITUO CHA AFYA MURIET - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 23 April 2020

DC AMPA SIKU 7 MHANDISI WA JIJI LA ARUSHA KUWEKA MAJI KITUO CHA AFYA MURIET

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini na kutoa siku Saba kwa mhandisi kuhakikisha wanaweka maji kwenye kituo Cha Afya huku akipongeza Ujenzi wa madarasa hayo na kutaka yakamilike kwa wakati picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Na Ahmed Mahmoud, Arusha

MKUU wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro ametoa siku saba kwa Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Samwel Mshuza kuweka maji katika jengo la upasuaji lililopo katika kituo cha afya cha Muriet ili kuanza shughuli za upasuaji.

Akizungumza katika siku ya pili ya ziara yake alipotembelea kituo hicho katika kukagua ujenzi wa njia ya kutembea kwa miguu inayounganisha majengo yote uliokamilika tarehe 4 Machi mwaka huu uliogharimu shilingi milion 100.

Mkuu huyo amesema kuwa anatoa siku saba kwa mhandisi huyo kwani maji ni sehemu kubwa ya kukwamisha  wananchi kupata huduma ya upasuaji pamoja na shughuli nyingine ndani ya majengo hayo. Akiwa katika shule ya sekondari Taret mkuu huyo amesema kuwa kabla ya mwaka wa fedha kuisha majengo hayo yawe tamekamilika ili kuanza mwaka mwingine wa fedha isiokuwa na Madeni ya nyuma.

"Haitaleta maana nzuri kuona tunaanza mwaka mwingine tukiwa na Madeni na kutokukamilisha baadhi ya majengo tunatakiwa kuanza mwaka na miradi mingine sio ya viporo". Alisema daqqaro

Hata hivyo Mkurugenzi wa jiji hilo, Maulid Madeni amesema kuwa jiji limesimamisha shughuli zote za kawaida ili kuweza kukamilisha majengo yote .

" Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunatambua wewe ni msaidizi wa Rais ndani ya eneo Hilo naomba nikuahidi jengo hili  ndani yasiku 30 litakuwa limekamilika".

Akizungumza mmoja wa wananchi wa eneo Hilo Abdala maguta amesema kuwa wanaishukuru serikali  kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuwarahisishia wanafunzi wengi kutokwenda mashule ya mbali .

No comments:

Post a Comment