PINGO'S FORUM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUPAMBANA NA COVID 19 WILAYANI SIMANJIRO MKOA WA MANYARA VYENYE THAMANI YA MILION 18.2 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 22 April 2020

PINGO'S FORUM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUPAMBANA NA COVID 19 WILAYANI SIMANJIRO MKOA WA MANYARA VYENYE THAMANI YA MILION 18.2

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Yafred Myezi akipokea vifaa vya mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19 kutoka kwa Mkurugenzi wa Pingo's Forum Edward Porokwa Kwenye makao makuu ya shirika hilo Sakina Jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Na Ahmed Mahmoud Arusha

SHIRIKA la Mtandao wa Wafugaji na Wawindaji sanjari na Waokota Matunda la PINGO'S limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 18.2 kuisaida Serikali kwenye mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa niaba ya jamii ya Wafugaji wilayani humo kwaniaba yao kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yafred Myenzi

Akiongea wakati akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Pingo's Edward Parokwa alisema kuwa wilaya hiyo imepakana na mikoa mitatu hivyo muingiliano huo unaifanya wilaya hiyo kuweza kupata kwa urahisi Ugonjwa huo.

Alisema jamii hiyo imekuwa ikiuza dawa za kienyeji maeneo mengi nchini na hata nje ya nchi hivyo uwezekano wa kuja na maambukizi ndio umepelekea wao kuanza nao kuwapatia vifaa vya kujikinga na Ugonjwa huo wa Covid 19.

Akabainisha idadi ya vifaa walivyokabidhi na lengo la kusaidia wilaya hiyo kuwa inamuingiliano wa wageni wanaotoka nchi jirani kufika kununua mifugo pia inapakana na mikoa minne ya Dodoma,Arusha,Kilimanjaro na Tanga kwa kuwa vijana wengi wanauza madawa maeneo mengi Kuna uwezekano wa kuja na magonjwa ya Covid 19.

"Jambo lililotufanya tuone umuhimu wa kupeleka vifaa hivi kwenye wilaya hii ni kutokana na muingiliano wa vijana wetu wengi wanafanya biashara ya kuuza dawa za kienyeji maeneo mengi nchini na nje ya nchi hivyo uwezekano wa kuja na maambukizi ni mkubwa"

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Elizabeth Oning'o alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na vitasaidia mapambano ya kukabiliana na Ugonjwa wa Covid 19 wilayani humo.

Alisema wilaya hiyo imekuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo kutokana na kuwa na migodi ya Tanzanite Jambo linalohitaji vifaa vya kujikinga na kwa Sasa vitasaidia kwa kuwa walikuwa na upungufu kwenye kambi zao na vituo vyao vya Afya wilayani humo. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Yafred Myenzi amelipongeza shirika hilo la Pingo's Forum kwa kuamua kusaidia wilaya hiyo kwenye mapambano ya janga la Ugonjwa wa Covid 19.

Alisema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya mwingiliano kutokana na wakazi wengi wanafanya shughuli zao nje ya wilaya hali inayotishia uwezekano wa kuwa na wagonjwa wengi.

No comments:

Post a Comment