TISHIO VIRUSI VYA CORONA, SALAM SASA NI KUGONGANISHA MIGUU....! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Wednesday, 4 March 2020

TISHIO VIRUSI VYA CORONA, SALAM SASA NI KUGONGANISHA MIGUU....!

Muuguzi Mfawidhi wa Kituo cha Afya Pugu Kajungeni, Bi. Sikudhan Yotham akiwamiminia kemikali maalum ya kukinga uenezaji wa virusi baadhi ya wageni waliotembelea kituo hicho, kufuatia ushauri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dk. Sophia Mjema (kulia) akisalimiana kwa ishara za kugonganisha miguu na baadhi ya wageni na wadau wa maendeleo walipokutana katika Kituo cha Afya cha Pugu Kajungeni jijini Dar es Salaam. Hii ni ishara ya kupokea ushauri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Muuguzi Mfawidhi wa Kituo cha Afya Pugu Kajungeni, Bi. Sikudhan Yotham akiwamiminia kemikali maalum ya kukinga uenezaji wa virusi baadhi ya wageni waliotembelea kituo hicho, kufuatia ushauri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa ishara ya mikono bila kugusana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokugusana mikono, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Salamu hiyo ya kutokugusana mikono ni kutekeleza ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment