Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiwa katika shule ya sekondari ya Ifunda Girls mkoani Iringa wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa akikagua miradi ya elimu na kutoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza.
Mkuu wa mka wa Iringa Ally Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya walipokuwa wanawasili katika shule ya sekondari ya Isimila kwa ajili ya kukagua miradi ya elimuna na kutoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Isimani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alipokuwa anatoa tamkoa la kila shule kuwa na chumba cha huduma ya kwanza.
NA FREDY
MGUNDA, IRINGA
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameziagiza halmashauri zote kuhakikisha zinajenga
chumba cha huduma ya kwanza kwenye kila shule ya sekondari kwa lengo la kuhudumia
wanafunzi wanaougua ghafla au wanaohitaji kupata huduma ya kwanza katika shule
hiyo.
Hayo
ameyazungumza wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa katika
shule ya sekondari ya Isimila alipokuwa anakagua majengo ya shule hiyo na
kubaini kuwa ni moja kati shule zenye chumba cha kutolea huduma ya kwanza kwa
wanafunzi na watumishi wa shule hiyo.
Alisema
kuwa kuna shule ambao zipo mbali na huduma ya afya hivyo wanapaswa kusafiri kwa
umbali mrefu,kuwepo kwa chuma hicho kusaidia kutoa huduma majira yote ya
usiku,mchana na asubuhi.
“Nimeona
shule nyingi hakuna magari ya wagonjwa wala chuma cha huduma ya kwanza hivyo
naagiza halmashauri zote kuhakikisha wanapojenga majengo ya shule lazima
wahakikishe wanajenga au wanatenga chumba maalumu kwa ajili huduma ya kwanza,”
alisema Hapi.
Hapi
aliagiza halmashauri zote kuhakikisha kuwa wanapojenga madarasa ya shule katikati yake lazima ijengwe ofisi ya
walimu kwa lengo la kuhakikisha walimu wanapata ofisi za kuwarahisishia kazi
wawapo shuleni hapo.
Aidha
mkuu wa mkoa aliagiza wakurugenzi wote kuhakikisha kuwa wanafunzi wote
waliofaulu wanaendelea na masomo na kuwakamata wazazi wote ambao hawataki
kuwapeleka wanafunzi shule kwa kuwa serikali inatoa huduma bure kuanzia shule
ya msingi na sekondari.
“Nataka
mhakikishe wanafunzi wote waliofaulu wanaenda shuleni kwa kufanya uchunguzi
maalumu,serikali inarusu mwanafunzi kuanza kusoma hata akiwa anadela,suruali
ambayo sio sare kwa kuwa serikali inalipa kila kitu kwa wanafunzi wote,” alisema
Hapi
Kwa
uapnde wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa uwepo wa
madarasa na mabweni kunachangia kuleta maendeleo ya mwanafunzi kwa kuongeza
ufaulu wa masomo yao hasa wanafunzi wa kike.
“Mheshimiwa
mkuu wa mkoa toka tumejenga madarasa haya mapya na mabweni kumekuwa na ongezeko
za ufaulu katika hiii ya shule na shule nyingi za wilaya hii hivyo nafikiri ni
jukumu letu kurudi kwa wananchi kuchangia maendeleo ya shule” alisema Kasesela
Kasesela
aliongeza kuwa bado kunachangamoto ya uhaba wa majengo ya madarasa katika shule
nyingi za sekondari za wilaya hiyo hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea
kuchangia matofali kwenye benki ya matofali ya kila kijiji.
No comments:
Post a Comment