Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini Donath Fungu akiendesha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang',Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uelewa dhidi ya athari za virusi vya Corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya kijinsia na kazi za nyumbani yaliyoandaliwa na shirika la Oxfam Tanzania.
Afisa Maendeleo ya jamii kutoka kata ya Kateshi wilayani Hanang' akichangia mada katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na shirika la Oxfam katika wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini Donath Fungu akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja.
Naelijwa Mshanga Afisa miradi kutoka shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini akifuatilia mafunzo yanayoendelea ya dhidi ya kujengewa ueklewa dhidi ya athari za virusi vya Corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya kijinnsia na kazi za nyumbani.
Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini Donath Fungu akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang',Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga.
Mzee wa kimila Thomas Madiye Sixista akiwa na mkalimani wake Albert Masuja akielezea namna wao wanavyoshiriki katika kutoa elimu kwa jamii namna ya kujikinga na maambukizi ya uvirusi vya corona.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayoendelea kutolewa.
Muendelezo wa mafunzo ya uelewa juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa watendaji wa vijiji na kata pamoja na wazee wa kimila ,watumishi wa Afya katika mkoa wa Manyara.
Daktari Giliad Zablon kutoka hospitali ya wilaya Hanang’Tumaini akiainisha baadhi ya dalili za Covid- 19 kwa washiriki wa mafunzo ya kujengewa uelewa yaliyoandaliwa na kuendeshwa na shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania .
Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam Tanzania kanda ya kaskazini Donath Fungu akiendesha mafunzo ya kuwajengea uelewa washiriki kutoka wilaya ya Hanang',Babati,na maafisa sekta ya afya mkoa wa Manyara dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga
Mmoja ya wazee wa kimila aliyehudhuria mafunzo hayo ya siku moja ya kujengewa uelewa dhidi ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga.
Na.Vero Ignatus,Manyara
OXFAM Tanzania imeendesha Mafunzo ya kujenga uelewa dhidi
ya athari za virusi vya corona na namna ya kujikinga ikihusishwa na maswala ya
kijinsia na kazi za nyumbani na kuwahusisha watendaji mbalimbali kutoka yaliyofanyika
Babati mjini ukumbi wa Good Life Hotel
Akizungumza Msimamizi wa miradi Shirika la Oxfam
Tanzania kanda ya kaskazini Donath
Fungu amesema kuwa shirika hilo limetengeneza utaratibu kwaajili ya
kukabiliana na majanga ,hivyo wameandaa mpango mkakati wa kujihadhari na
kutambua ugonjwa huo una athari kiasi gani katika jamii na namna ya kukabiliana
nao
Fungu amewataka
viongozi wote walioshiriki mafunzo hayo kuhakikisha kuwa jamii kwa ujumla ambayo
inahisiwa ipo katika mazingira hatarishi wanakuwa na taarifa
katika lugha ya kuaminika na taarifa hizo zitoke katika chanzo sahihi na
kuepuka habari zinazoleta taharuki zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Daktari Giliad
Zablon kutoka hospitali ya wilaya Hanang’Tumaini ameainisha baadhi ya dalili za
Covid- 19 kuwa ni pamoja na homa, joto la mwili kupanda,mwili kuchoka,kupumua
kwa shida,viungo kuuma,kichwa kugonga,mafua,kichefuchefu au
kutapika,kuhara,vidonda vya koo,kikohozi wakati mwingine makohozi
yanachanganyika na damu.
Amesema ni vyema kila mwanajamii ajenge tabia ya
kunawa mikono marakwa mara kwa maji tiririka na waepuke kusalimiana kwa kushikana
mikono pamoja na kukumbatiana
Kwa upande wake Katibu wa Afya mkoa wa Manyara Evance
Simkoko amesema kuwa wameainisha sehemu maalum za kuwatenga wale wote
wanaohisiwa kuwa na dalili za covid-19 kwaajili ya kuchukuliwa sampuli.
Simkoko ameeleza juu ya serikali ya mkoa huo kudhibiti
upandaji holela wa vitakatishi vya mikono pamoja nan doo zinazoandaliwa
kwaajili ya maji ya kunawa katika maeneo mbalimbali.
Mafunzo hayo yamewashirikisha wenyeviti wa serikali za
vijiji,wazee wa Kimila wataalamu wa afya
,Maafisa maendeleo ya jamii wilaya Mafisa ustawi wa jamiii,pamoja na madaktari
wa binadamu ambapo waliendesha kikao
hicho kwa njia ya majadala
Akizungumza kwa niaba ya wazee wa kimila Mzee Thomas Madiye Sixista amesema kuwa imekuwa ni changamoto kwa wazee hao kuifikia jamii kutoa elimu kutokana na kuzuiliwa kwa mikusanyiko ingawa wanaipongeza serikali kwa hatua walizozichukua na utoaji wa elimu unaoendelea katika jamii
Madiye amesema kuwa japokuwa elimu bado inahitajika kwani bado kwenye magari ya usafiri wa abiria wameendelea kujaza abiria kupita uwezo wa gari
Aidha hadi sasa serikali imechukua jitihada mbalimbali
za kuhakikisha wananchi wanajiepusha na maambukizi imeweka utaratibu kwenye
viwanja vya ndege,kuzuia vibali vya
kusafiri nje yan chi, kufunga shule zote za msingi na vyuo,kuepuka mikusanyiko
isiyokuwa ya lazima, kuhakikisha kuwa kila mwananchi ananawa mikono kwa usalama
wake.
No comments:
Post a Comment