NMB YACHANGIA MILIONI 100 KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 30 March 2020

NMB YACHANGIA MILIONI 100 KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA

Waziri Mkuu - Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) akipokea hundi ya Sh. Milioni 100 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna (wa nne kutoka kushoto) Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Serikali wa NMB Alfred Shao na kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Ummy Mwalimu.

BENKI ya NMB imechangia kiasi cha kifedha shilingi Milioni 100 kama msaada kwa Serikali ikiwa ni kushirikiana kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona. Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna amekabidhi msaada huo kwa Mhe. Waziri Mkuu - Kassim Majaliwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali. Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa akizungumza na uongozi wa Benki ya NMB.

Benki ya NMB ikiwa na maadhimio sawa ya kuudhibiti ugonjwa huu, mchango huu utaisaidia serikali katika mapambano dhidi ya virusi hivi. Tunasisitizwa kuendelea kutumia njia stahiki kujikinga na maambukizi.

No comments:

Post a Comment