MKURUGENZI
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimueleza jambo Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma Zainabu
Vullu kulia wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la Tanki la Maji
litakalotoa maji eneo la Pongwe kupeleka wilayani Muheza wakati wa
ziara yako wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt
Fungo Ally.
MKURUGENZI
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati akisisitiza jambo kwa kamati hiyo.
MKURUGENZI
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Zainabu Vullu kulia ni mjumbe wa kamati hiyo wakati
wakiingia kwenye mradi huo.
Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea maeneo mbalimbali katika mradi huo
AFISA
Uhusiano wa Tanga Uwasa Devota Mayala kushoto akimsikiliza kwa umakini
mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo wakati walipotembelea mradi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma Zainabu Vullu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati hiyo kutembelea mradi huo.
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akielezea mradi huo
wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma.
MRADI
wa Maji kutoka Pongwe Kitisa Jijini Tanga hadi wilaya ya Muheza
umeelezwa kwamba umefikia asilimia 90 ya ukamilifu wake huku kazi chache
zilizobakia ni kufunga pampu.
Mradi huo utakapokamilika unaelezwa kwamba utakuwa mkombozi mkubwa kwa
wilaya ya Muheza na maeneo ya jirani ambako mradi huo utapita kuelekea
wilayani humo na hivyo kuondosha kero ya kutokupatikana huduma hiyo
muhimu.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa
ziara ya Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma ilipotembelea
mradi huo na kujionea namna ulivyotekelezwa huku wakiridhishwa na namna
ulivyotekelezwa.
Alisema
kwa sasa masharti ya mkandarasi na msambazaji wamekubaliana msambazaji
azifunge pampu hizo ili ziweze kuwa na muda wa matazamio kuwa na uhakika
kwa kipindi chote ambacho wamekubaliana.
Aidha alisema kwa sababu pampu walizokubaliana ni kubwa na gharama kubwa
ambazo gharama zake ni zaidi ya milioni 100 hivyo isipokuwa na muda wa
matazamio ni hatari sana kwa uendelevu wa mradi.
Mkurugenzi
huyo alisema changamoto kubwa ilikuwa ni malipo na sasa yamepatikana
kwa hiyo wanategemea mkandarasi anawasiliana na mzabuni wa pampu ili
aweze kufikia kuzifunga hizo na mwishoni wa mwezi wanne katikati inaweza
mradi ukawa umekamilika na maji kufika Muheza.
“Tunaishukuru
serikali wakati inaoingia madarakani walikuwa na ilani ambayo
ilitarajia kufikisha huduma kwa wananchi katika mwaka 2017 walianzisha
mradi huo kupeleke maji Muheza na kwa sababu hali ya Muheza ilikuwa
mbaya siku nyingi”,Alisema.
“Kwani
upatikanaji wake ni asilimia 35 kwa hiyo mradi huo baada ya ukamilifu
wake utafanikisha kifikia asilimia 65 na kuna kazi ndogo za kufanyika
ikiwemo kufumua miundombinu ya maji Muheza na ikikamilika itapelekea
upatikana na maji kufikia asilimia 85 hadi 90”,Alisema.
Awali
akizungumza wakati alipotembelea mradi wa Pongwe Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Zainabu Vullu alisema kwamba wao kama kamati wameridhishishwa na
mradi huo na kwamba kama walivyoelezwa kwamba utawanufaisha wananchi.
Alisema
kamati zote kwenye kipindi hiki kabla ya bajeti inapita kwenye maeneo
mbalimbali kuangalia miradi ambayo serikali imewekaza ili kuona maslahi
na manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi.
Alisema ziara yao ni moja ya kutimiza kanuniz za kibunge kuangalia jinsi
gani serikali imewekeza na leo wameona jinsi serikali imewekeza wana
tenki la lita laki saba ambalo litasaidia pia na vijiji jirani ili
kuweza kunufaika na mradi huo .
“Niseme kwamba sekta ya maji ni muhumu sana kwa maisha ya mtanzania na
inatakiwa kumtua mwanamke ndoo kichwani aweze kufanya kazi nyengine za
uzalishaji manufaa ya tenki hilo sio wananchi hata viwanda
vitakapoanzishwa watapata maji kutoka hapo hapo”Alisema
No comments:
Post a Comment