MATUKIO PICHA : MAJALIWA APOKEA MISAADA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 28 March 2020

MATUKIO PICHA : MAJALIWA APOKEA MISAADA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mikono wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajil ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipima joto la mwili wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakikagua jenereta lilitolewa na familia ya Karimjee  Jivanji ya jijini Dar es salam lenye thamani ya sh. milioni 75 wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili  ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azan Zungu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu,   Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 230  ukiwa ni mchango wa Benki ya UBA wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Usman Isaka na wa nne kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Farhiya Warsama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment