MATUKIO PICHA : KAMATI YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA YASISITIZA VIWANGO VYA UBORA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 14 March 2020

MATUKIO PICHA : KAMATI YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA YASISITIZA VIWANGO VYA UBORA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, akijaribu ubora wa mataruma yanayotengenezwa katika Kiwanda cha Mataruma Kilosa, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea na kukagua mataruma yanayozalishwa katika Kiwanda cha Kilosa, Mkoani Morogoro.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (wa pili kulia) na wajumbe wa kamati hiyo, wakati ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment