IGP Sirro akiwa na mfadhili huyo Fouad Martis na Mkuu wa mkoa wa Arusha wakitembelea majengo hayo ya makazi ya Askari wa jeshi la Polisi ambayo yanatarajiwa kukamilika mwezi wa nne mwaka huu. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la polisi nchini limewaonya viongozi wa madhehebu ya dini kutoingilia mambo ya kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwani halitasita kumchukulia hatua kali yeyote Yule atakayekiuka agizo hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro aliyasema hayo juzi alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jingo la nyumba za Askari polisi zinazoendelea kujengwa katika eneo la kikosi cha kutuliza ghasia FFU kata ya Muriet jijini Arusha.
Alisema kuwa kila kiongozi wa imani ya madhehebu yoyote ya kidini antakiwa kufanya shughuli zake katika eneo lake la kazi na kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana na yeyote Yule atakayesababisha kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani na utalivu hapa nchini.
“Wewe kama askofu,Mchungaji Padri au Sheikh shughuli zako za kiimani zifanye kanisani au msikitini na hata wewe mwananchi fanya shughuli zako bila kutenda au jaribio la kiuhalifu sisi hatutojali endapo utaenda kinyume na taratibu zilizopo tutakufikia na kukukamata popote ulipo kwani hakuna aliye juu ya sheria”alisisitiza
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi aliwataka askari polis nchini kuhakikisha wanafanyakazi zao kwa weledi uaminifu na watende haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya kutokutenda haki kwa baadhi ya askari hao hivyo wazingatia kiapo chao kwenye utendaji wao wa majukumu ya kila siku.
Akatoa wito kwa wananchi wote nchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu watende na kufanya shughuli halali ambapo amekemea tabia ya wazazi na walezi ambao wamekuwa wakiwatetea watoto wao wanajihusisha na matukio ya kiuhalifu hivyo amewataka kuwalea kwenye maadili mema.
Awali akimkaribisha IGP mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alilipongeza jeshi hilo mkoani hapa chini ya usimamizi wa kamanda wa polisi mkoani hapa Jonathan Shana kwa usimamizi mzuri na kupambana na uhalifu mkoani hapa.
Kadhalika Gambo alimuomba mkuu wa jeshi la polisi kukipandisha hadhi kituo cha polisi Muriet ambapo hapo hapo Sirro alikubali ombi hilo na kukipa hadhi kituo hicho kuwa kituo cha polisi cha kiwilaya Muriet na ataleta OCD na OCS katika kituo hicho ili wananchi wapate huduma za kipolisi kwa kuwa kuna wananchi wengi na huduma nyingi wanapata kituo kikuu cha polisi jijini Arusha.
Akaahidi kuhakikisha kuwa wanaendeleza kuuweka mkoa huo kuendelea kuwa salama na Amani ambapo pia akawataka wananchi mkoani hapa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwenye mapam,bano ya kiuhalifu kwa kutoa taarifa za kiuhalifu.
“IGP Sirro naliomba jeshi la polisi mjenge mazingira mazuri kwa askari kuwajengea makazi na kuboresha maslahi yao kwani kwa kufanya hivyo askari watakuwa na morali ya kufanyakazi hivyo uhalifu hautakuwa na nafasi mkoani hapa na nchini kwa ujumla wake”alisema
Kwa Upande wake Balozi wa Heshima wa serikali ya Dubai Fouad Martis ambao ndio wafadhili wa mradi huo wa nyumba za polisi wenye thamani ya dola za kimarekani laki mbili alisema kuwa wao kama wawekezaji hapa nchini wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni kurudisha kwa jamii faida kidogo wanayoipata.
Nae Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya CRJE ya China Tumainiel Seria alisema kuwa jengo hilo lina nyumba sita ikiwemo sebule,vyumba viwili vya kulala na jiko na kwamba ujenzi umefikia asilimia 50 na wanaahidi kuukamilisha mwezi wa nne mwaka huu.
No comments:
Post a Comment