Wakili Suzana Senso akizungumza wakati akitoa mada
ya nafasi ya mwanamke kwenye urithi wa mirathi maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Nkende Manispaa ya Musoma mjini
iliyokuwa na kauli mbiu ya Kizazi cha Usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya
Sasa na ya Baadae.
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo kushoto ni Mwenyekiti wa UWT
Taifa Gaudance Kabaka akifuatiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Caroline Matapula na Mkurugenzi wa Musoma Mjini Mjovela na kulia ni Wakili Suzana Senso.
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.
Wakili Suzana Senso wa pili kutoka kulia akishiriki kucheza na wakina mama wengine wakati wa maadhimisho hayo.
WAKILI Suzana Senso amesema kwamba hata wanawake wanaweza kuandika mirathi ili kupunguza msongamano wa kesi za kugombania mali kwenye jamii pindi wanapokuwa wakitangulia mbele za haki.
Senso aliyasema hayo wakati akitoa mada ya nafasi ya mwanamke kwenye urithi wa mirathi huku akisisitiza wanawake kujituma na kutafuta mali kutokana na kuwepo kwa dhana potofu kwamba wanapotafuta hakuna watakaonufaika na mali hizo pindi wanapofariki .
Maadhimisho ya siku ya wanawake dunia iliyofanyika kwenye viwanja vya Nkende Manispaa ya Musoma mjini iliyokuwa na kauli mbiu ya Kizazi cha Usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya Sasa nay a Baadae.
Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudance Kabaka ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Caroline Matapula,Madiwani wa Viti Maalumu wa Manispaa ya Musoma,Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa huo na Mwakilishi wa Mbunge Anna Makilanga na Mwakilishi kutoka Takukuru.
Wakili Senso alisema kwamba sheria ya mirathi inasema kama mke akifariki na kumuacha mume na watoto mume hupata moja ya tatu ya mali za marehemu mkewe na mbili ya tatu huenda kwa watoto.
Alisema kwamba pia ikitokea mke amefariki na amemuacha mume lakini hakuna watoto inaangaliwa kama kuna ndugu ikiwa wapo ndugu hao wa mke hutakiwa kupata nusu ya mali na nusu inayobakia huenda kwa mume kwa hiyo ndugu wa mwanamke ambao ni marehemu hupata sawa kwa sasa na mume wake aliyeachwa.
“Lakini ikiwa mwanamke ndiye amefariki na hakuacha ndugu yoyote wala mtoto yeyote isipokuwa kumuacha mume haturudhi mali zote za Mkwe”Alisema
Akizungumza katika maadhimisho yalikwenda sambamba na wakina mama wajasiriamali kuonyesha bidhaa zao ambapo mgeni rasmi Mama Kabaka alionyesha kufarijika alipokuta wakina mama wanapiga vita umaskini kwa kujishughulisha na biashara.
Pia maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Benki tofauti tofauti ikiwemo NMB, NBC na Kampuni za simu ikiwemo TTCL pia kwenye maonyesho hayo kulikuwa na dawati la jinsia ambalo lilitoa elimu kwa wananchi walikuwa wamehudhuria.
No comments:
Post a Comment