Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino Jijini Roma, Nchini Italia kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa IFAD. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino Jijini Roma, Nchini Italia kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa IFAD
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
WAZIRI wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 10 Februari 2020 amewasili Jijini Roma nchini Italia na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Flumicino.
Mhe Hasunga amezuru nchini Italia ambapo atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Mkutano huo ambao hufanyika mwezi Februari ya kila mwaka na huongozwa na Rais wa IFAD na kuhudhuriwa na Magavana wan chi wanachama ambao ni Mawaziri wenye dhamana ya Kilimo.
Mkutano huo wa Magavana wa IFAD ndio chombo kikuu chenye maamuzi ya ngazi ya juu (High Level Decision Making Body) kuhusiana na shughuli zote za IFAD kwa kipindi cha mwaka mzima, Hivyo Waziri wa Kilimo wa Tanzania ni Gavana wa Tanzania ambaye pia ana dhamana ya kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo muhimu.
Kauli mbiu ya Mkutano wa 43 wa Magavana wa IFAD ni “Kuwekeza katika Mifumo Endelevuya Chakula kwa ajili ya kusitisha njaa ifikapo mwaka 2030 – Investing in sustainable food systems to end hunger by 2030”.
Majadiliano ya mkutano huo utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Februari 2020 yamelenga kuhakikisha ni kwa jinsi gani IFAD itaweza kutumia uzoefu wake katika masuala ya chakula na lishe ili kuweza kufikia lengo la pili la Maendeleo endelevu ya Dunia la kutokuwa na njaa kabisa (SDG 2 – Zero hunger).
IFAD ni Shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo, ambalo ni shirika la Umoja wa mataifa kwa ajili ya maendeleo vijijini lilioanzishwa tarehe 13 Desemba 1977 kwa lengo kufanya ukue uzalishaji wa kilimo na vyakula haki kufikia kwa ngazi ya maisha ya kujitosheleza.
Kwa namna hiyo unafadhili wa mipango ya kimaendeleo na ambayo ni muhimu kwa masikini zaidi kati ya masikini duniani na ambao wanaishi katika vijijini pembezoni kabisa mwa miji. Ni 70% ya watu duniani mara nyingi wamesahuliwa na wenye kuhitaji msaada mkubwa.
No comments:
Post a Comment