Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus Nyongo akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Madini wa Uganda Bi.Sara Nkoniakizungumza katika mkutano huo.

Katibu Mkuu wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifurahia hotuba ya Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko wakati alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) akifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa kwenye mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Washiriki mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko akiwa meza kuu pamoja na waziri wa Madini wa Uganda Bi.Sara Nkoni pamoja na mawaziri na viongozi mbalimbali wanaoshughulikia madini
![]() |
| Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada wakati zikiwasilishwa. |
WAZIRI
wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa cheti cha kuuza na kusafirisha
madini ya bati nje ya nchi kitatolewa kesho na kueleza kuwa cheti hicho
ni hatua kubwa kwa wachimbaji wa madini nchini katika kukuza na
kuimarisha sekta hiyo muhimu.
Akizungumza
na wawekezaji katika sekta ya madini katika kituo cha kimataifa cha
mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo jijini Dar es Salaam Biteko
amesema Serikali ipo pamoja na wachimbaji hao hasa kwa kushirikiana nao
ili kuendeleza sekta hiyo adhimu.
"Mkutano
huu ni wa kutangaza fursa na kubwa zaidi ni kesho ambapo tupokea cheti
cha kusafirisha madini ya bati nje ya nchi kibali ambacho hatukuwa nacho
awali" ameeleza Biteko.
Pia
amesema mafanikio katika sekta hiyo ni makubwa na yenye tija kwa taifa
kwani hata ukusanyaji mapato kwa sasa mapato yanayokusanywa yamefikia
zaidi ya shilingi bilioni 300.
Awali
akizungumza wakati wa warsha hiyo Mwenyekiti wa Shirikisho la
wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) John Nina ameipongeza
Serikali kupitia Wizara ya madini kwa kuonesha ushirikiano hasa katika
utatuzi wa changamoto.
"
Changamoto zilizokuwa zinatukabili zimetatuliwa kwa asilimia 80 na
tunafurahi kwa sasa Sheria ya madini ni faaafu na Tanzania ni sehemu
salama ya uwekezaji" Ameeleza Shayo.
Aidha
amewataka wachimbaji hao kushirikiana katika kuendeleza sekta hiyo na
kueleza kuwa ikitokea kukawa na siku ya madini, wachimbaji wamependekeza
siku hiyo iitwe Magufuli Minerals Day na hiyo ni kutokana na mchango
mkubwa wa Rais Magufuli katika kuinua na kuweka mazingira bora kwa
ukuaji wa sekta hiyo.
Mkutano
huo wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka
2020 uliobeba kauli mbiu ya "Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya
madini" umehudhuriwa na mawaziri wa madini kutoka nchi mbalimbali Afrika
ikiwemo Uganda na Congo na utafungwa kesho na waziri Mkuu Kassim
Majaliwa.


No comments:
Post a Comment