Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga Solomon Mwangamilo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa shule za msingi na sekondari Jijini Tanga |
Mkurugenzi wa Asasi inayojishughulisha na Usalama Barabara ya Amend Tom Bishop akizungumza wakati wa halfa hiyo |
MWAKILISHI
wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo ambaye ni Diwani
wa Kata ya Mzingani na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Mazingira wa pili kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi huo
MWAKILISHI
wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo ambaye ni Diwani
wa Kata ya Mzingani na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,Afya na Mazingira
wa pili kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi huo.
MEZA Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo
SEHEMU ya wanafunzi wa shule za Msingi Chuma, Masiwani,Kana na Shule ya Sekondari Maawal.
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kushoto akiwa na Mwakilishi wa Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo akiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga
Solomon Mwangamilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa
shule za msingi na sekondari Jijini Tanga.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo
UDHIBITI wa makosa ya usalama barabara mkoani Tanga umesaidia kupunguza matukio ya ajali zilizohusisha watoto kutoka 41mwaka 2018 hadi kufikia ajali 9mwaka 2019.
Takwimu
hizo zimetokewa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga
Solomon Mwangamilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa usalama barabara kwa
shule za msingi na sekondari Jijini Tanga.
Alisema
kuwa ukaguzi wa Mara kwamara ya vyombo vya moto pamoja na elimu ya
usalama barabara ndio imeweza kusaidia kupunguza ajali hizo.
"Changamoto
pekee iliyobaki kwa Sasa ni watoto chini ya miaka 9 kupakiwa kwenye
usafiri wa bodaboda zaidi ya watatu kwa ajili ya kupelekwa shule Jambo
ambalo ni hatari kwa usalama wao "alisema RTOMwangamilo.
Aidha
alisema kuwa kupitia mradi huo anaamini utaweza kuja na suluhisho la
kumaliza ajali za barabara kwa wanafunzi hususani katika shule ambazo
zipo karibu na maeneo yabarabara kuu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa asasi inayojishughulisha na usalama barabara
Amend Tom Bishop alisema kuwa mradi huo utasaidia kujenga vivuko katika
maeneo ya shule pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya barabara kwa
wanafunzi.
"Tunajua
kwamba maendeleo ya miji mikubwa duniani inakuja na changamoto ya
ongezeko la ajali hivyo kupitia mradi huu tumekuja kusaidiana na
serikali katika kuhakikisha ndoto ya mtoto wa kitanzania
inatimia"alisema Bishop
Nae
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kuwa mradi kupunguza
ajali ambazo walikuwa wanapata wakati wanapokwwnda shule na wanaporudi
nyumbani.
"Sasa Kuna njia
maalum ya kupitia waenda kwa miguu kwani awali vyombo vya moto na
watembea kwa miguu walikuwa wanatumia kwa pamoja na hivyo kuweka hatari
ya uwepo wa ajali"alisema Mayeji
No comments:
Post a Comment