HELIKOPTA ILIYOMBEBA KOBE BRYANT HAIKUWA NA UWEZO WA KUSAFIRI KWENYE UKUNGU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 1 February 2020

HELIKOPTA ILIYOMBEBA KOBE BRYANT HAIKUWA NA UWEZO WA KUSAFIRI KWENYE UKUNGU



Bryant alikuwa bingwa mara tano wa mchezo wa kikapu NBA kwa timu yake, Los Angeles Lakers

SHIRIKA la Island Express Helicopters linalomiliki helikopta iliyombeba mchezaji mpira wa kikapu Kobe Bryant, binti yake na watu wengine 7 wakati iliyoanguka, halikuwa na ruhusa ya ndege zake kusafiri katika sehemu zenye ukungu, maafisa wamesema.

Shirika la Island Express lilikuwa na ruhusa ya ndege zake kusafiri wakati rubani anaweza kuona vizuri kule anakoelekea na hali ya hewa ni shwari.

Inasemekana kwamba rubani wa ndege iliyoanguka, alikuwa na cheti cha kuendesha helikopta kwa kuzingatia vifaa vya chumba cha rubani pekee.

Hata hivyo imesemekana kwamba huenda alikuwa na uzoefu mdogo katika hilo, mtaalam amesema.
Hii ilikuwa ni kwasababu ya masharti yaliyokuwepo dhidi ya kampuni.

Sababu ya ajali hiyo ambayo ni hali ya hewa ya ukungu magharibi mwa Los Angeles bado inachunguzwa.

Bryant alikuwa anasafiri kama kocha wa binti yake aliyekuwa anashiriki mashindano ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana katika chuo cha michezo cha Mamba.

Wakati huohuo, Ijumaa timu ya Lakers ilishiriki mchezo wake wa kwanza tangu Bryant alipoaga dunia dhidi ya timu ya Portland Trail Blazers katika uwanja wa Staples LA.

Timu hiyo ilitoa heshima zake kwa Bryant kwa kuvalia jezi zake namba 8 na 24 huku maelfu ya mashabiki wakipaza sauti na kusema, "Kobe, Kobe!"

Timu ya Lakers ilitoa heshima zake kwa Bryant kwa kuvaa jezi zake namba - 8 na 24 - wakati wanapasha misuli moto

Mwimbaji maarufu Usher kisha akaanza kuimba wimbo wa Amazing Grace, na kupanga mashada ya maua kwa maumbo ya namba 8 na 24.

Wakati anatoa heshima kwa nyota huyo, mchezaji mahiri wa Lakers LeBron James aliambia hadhira: "Ukweli wa kwamba niko hapa, kwangu ina maana kubwa sana.

"Tutaendeleza alichoacha Bryant mimi pamoja na wachezaji wenzangu siyo tu kwa mwaka huu lakini mradi tunaendelea kucheza mchezo huu wa mpira wa kikapu ambao tunaupenda sana, kwasababu hilo bila shaka ndilo ambalo Kobe Bryant alitaka kufikia."


Kipi zaidi kinachofahamika kuhusu ajali ?
Helikopta za shirika la Island Express zilikuwa zinaruhusiwa kufanya safari chini ya kile kilachofahamika kama sheria ya ndege katika kuona, kwa maana kwamba rubani ni lazima awe anaona vizuri hali ilivyo kwa nje wakati wa mchana, Keith Holloway, msemaji wa Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafiri wa Ndege amezungumza na shirika la habari la Reuters.

Shirika hilo halikuruhusiwa kusafiri kwa kutumia vifaa vya kwenye chumba cha ndege pekee.
Bwana Holloway amesema haijafahamika ikiwa rubani, Ara Zobayan, alikuwa kwenye chumba cha rubani wakati ajali inatokea.

Bwana Zobayan alikuwa anaruhusiwa kusafiri kwa kutumia vifaa vya chumba cha rubani, Kurt Deetz, aliyekuwa rubani wa kampuni hiyo ambaye alimsafirisha Bryant kwa miaka miwili amezungmza na Forbes.

Hata hivyo, aliongeza: "Sidhani kama alikuwa na tajriba yoyote ya kuendesha ndege ndani ya mawingu."

Shirika la Island Express lilirejelelea ombi la kuzungumzia ajali hiyo la Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafiri wa Ndege.

Alhamisi, kampuni hiyo ilisema kwamba inasitisha huduma zake.

"Ajali hiyo ilipokelewa kwa mshtuko mkubwa na wafanyakazi wote na kampuni imeamua kwamba itasitisha huduma zake hadi wakati ambao utakuwa mwafaka kwa wafanyakazi na wateja," Shirika hilo limesema.

Ripoti ya awali ya ajali hiyo inatarajiwa kutoka ndani ya siku kumi.


Helikopta hiyo - Sikorsky S-76B - ilianguka milimani nje ya mji wa Calabasas Jumamosi asubuhi.
Hali ya hewa ilikuwa ukungu wakati inapaa na polisi wa eneo walikuwa wamesitisha safari za helikopta zao kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

Rubani aliomba wadhibiti wa ndege ruhusa maalum ili aweze kusafiri kwa hali ya hewa ambayo siyo ya kuridhisha, mwanachama wa Bodi ya usalama wa safiri wa ndege Jennifer Homendy, ambaye pia alihudhuria eneo la tukio kuchukua ushahidi amesema.

Helikopta hiyo, aliongeza, ilizunguka kwenye anga kwa dakika 12 kabla ya kupata ruhusa. Kisha rubani huyo akaomba wadhibiti, kumfuatilia, usaidizi unaotolewa kwa helikopta kuepusha mgongano, lakini akaarifiwa kwamba ndege hiyo ilikuwa chini mno na haikuweza kuonekana kwenye rada.

Dakika chache baadae, rubani alisema anendelea kupaa kuepuka ukungu wa mawingu mazito", aliongezea. Helikpta hiyo ilipanda na kuanza kushuka upande wa kushoto, kulingana na data ya rada, kabla ya mawasiliano kupotea tukio linaloendana na eneo ajali ilipotokea.

-BBC

No comments:

Post a Comment