ODION IGHALO: MSHAMBUALIAJI WA NIGERIA ALIYESAJILLIWA NA MANCHESTER UNITED - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 1 February 2020

ODION IGHALO: MSHAMBUALIAJI WA NIGERIA ALIYESAJILLIWA NA MANCHESTER UNITED

Odion Ighalo aliondoka Watford na kwenda China mwaka 2017


MANCHESTER United imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Watford Odion Ighalo kutoka Shanghai Shenhua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Makubaliano ya kumsajili mchezaji wa kimataifa Ighalo, 30, Old Trafford inakuwa haina chaguo jengine zaidi ya kumnunua.

Ighalo, ambaye bado yuko China anatarajiwa kusafiri kwenda Uingereza ndani ya siku chache zijazo, alifunga mabao 39 katika mecho 99 alizocheza Watford kati ya mwaka 2014 na 2017.

"Odion ni mchezaji mwenye tuzoefu mkubwa," amesema mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer.

"Ataingia na kuongezea idadi ya washambuliaji tulionao katika kipindi kifupi atakachokuwa nasi.''

"Mchezaji mahiri sana katika kazi yake, atakuwa na manufaa makubwa hapa." alisema Solskjaer.

Odion Ighalo ni nani?

Ighalo alijunga Super League ya China mwaka 2017, kwanza akiwa na timu ya Changchun Yatai.

Baada ya misimu miwili, akajiunga na timu ya Shanghai Shenhua na kufunga mara 10 katika mechi 19 ambazo alishiriki.

Aidha,Odion Ighalo alikuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la Afrika kwa kufunga mabao 7 kabla ya kufunga matano katika mashindao ya msimu wa joto.

Inafahamika kwamba klabu za ligi nyengine za Premier pia zilikuwa zimeonesha nia ya kumsajili Ighalo lakini mwenye alitaka kucheza na United.

Ighalo ni mchezaji wa waknza kusajili kwa mkopo wa aina hiyo tangu kuwasilis kwa Radamel Falcao kutoka Monaco mwaka 2014.

Ighalo (kushoto) alipigwa picha akiwa amevalia fulana ya Manchester United wakati akiwa mtoto


Mapema Ijumaa, United ilifunga mpango wake wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth, Josh King badala yake ikamchukua mlinda lango Nathan Bishop kwa kima cha pesa ambacho hakikuwekwa wazi.

United kumkubali Ighalo haku wendani na sera ya United ya kusajili wachezaji kwa muda mrefu kama vile Bruno Fernandes, aliyahamia Old Trafford kutoka Sporting Lisbon Alhamisi.

Hata hivyo, hatua hii imechukuliwa ili kuziba pengo la Marcus Rashford aliyepata jeraha na United haingeweza kumaliza msimu bila ya kutafuta mtu atakayechukuanafasi yake.

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Rashford, 22, amekuwa nje kwasababu ya jeraha alilopata mgongoni baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba wakati wa Kombe la FA dhidi ya Wolves Januari 15.

Mwaka uliopita, Odion Ighalo alikataa ofa ya Barcelona

Mwandishi wa BBC John Bennett:
Mwaka 2015 baada ya timu ya Watford kupandishwa daraja, Ighalo aliulizwa iwapo angependa kujiunga na timu gani katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi ya Premier.

Bila kusita: "Old Trafford. Itakuwa ni ndoto iliyotimia iwapo nitakuja kucheza dhidi ya Manchester United, timu niliyokuwa naishabikia nikiwa kijana". Hakuwa na ufahamu wa kile kitakachotokea miaka 5 baadae.

Odion anajishirkisha kwa kiasi kikubwa tu na masuala ya kusaidia wengine nchini Nigeria na bado ni mshambuliaji mwenye kipaji.

Hatua iliyochukuliwa na United sio ya kawaida na nina uhakika kwamba mumesoma na kusikia mambo mengi yenye mtazamo hasi na ili kuwa na uwiano acha na mimi niwape yenye mtazamo chanya: Ighalo ni mchezaji namba 9 kwa kipaji cha kizaliwa na mfungaji magoli mwenye kasi na nguvu.

Barcelona ilijaribu kumsajili miezi 12 iliyopita kwasababu walitaka mchezaji wa aina hiyo lakini akakataa ofa yao.

Odion Ighalo ni mchezaji mahiri na mwenye kuhimili changamoto. Nchini Nigeria alikosolewa vikali baada ya kukosa nafasi za kufunga kama mchezaji wa Super Eagles ambapo timu hiyo ilibanduliwa na Argentina katika mashindano ya kombe la Dunia mwaka jana lakini alipita jaribu hilo na kulimaliza akiwa mshindi zaidi baada ya kuwa mfungaji bora sio tu kwa Mashindano ya Kombe la Afrika bali pia katika mchezo wenyewe na kuwapiku wachezaji wengine mahiri kama vile Sadio Mane, Mohamed Salah na Riyad Mahrez.

Bila shaka ni mchezaji atakaye pambana kuhakikisha anakuwa na mafanikio makubwa ndani ya United.

Pia, kujiunga kwake United ni sawa na kurejea nyumbani kwasababu familia ya Ighalo imekuwa ikiishi Manchester.

Na hatua hii ni historia kubwa kwa mashabiki wa United kutoka Lagos.

Sasa wakati umewadia wa kuona ikiwa kwa mara ya kwanza katika taaluma yake, atadhihirishia umma kuwa anaweza.

'Ni shabiki wa United tangu akiwa mtoto

Mwandishi wa Nigeria Oluwashina Okeleji:
Miaka 5 baada ya mashabiki wa soka Nigeria kushuhudia kushindwa kwa mchakato wa kumsajili John Mikel Obi katika timu ya Manchester United, raia wa nchi hiyo hatimaye wana fursa ya kumshuhudia mchezaji wao mwenyewe akichezea timu ya Red Devil.

Akiwa na umri wa miaka 30, Odion Ighalo amekuwa mchezaji wa kwanza wa timu ya Super Eagle kujiunga na Old Trafford.

Ighalo akiwa alizaliwa katika eneo maskini la, Ajegunle, amekuwa shabiki wa United tangu akiwa mtoto.

Mashabiki wa taifa hilo la magharibi mwa Afrika, wanafuatilia kwa karibu Ligi ya Premier, ambayo imesajili baadhi ya wachezaji wazuri kutoka bara la Afrika.

-BBC

No comments:

Post a Comment