CHAMA CHA MAPINDUZI CHATOA SIKU 30 KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILINDINI – MICHEWENI, KASKAZINI PEMBA - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Friday, 21 February 2020

demo-image

CHAMA CHA MAPINDUZI CHATOA SIKU 30 KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILINDINI – MICHEWENI, KASKAZINI PEMBA

5R7A9709
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole


AKIWA katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya ya Micheweni leo tarehe 21 February 2020, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimetoa siku 30 kukamilishwa kwa mradi wa maji Wilaya Micheweni Pemba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Polepole kufika katika eneo la Kilindini ambapo kuna chanzo cha maji kinachopasa kupeleka maji kwa kilometa 4.6 hadi eneo la Micheweni lakini mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na kuelekeza kukamilika kwa haraka kwa mradi huo wa maji ili kurahisisha huduma za kijamii na Kiuchumi katika Wilaya ya Micheweni.

Aidha Ndugu Polepole ametembelea katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kije iliyopo Jimbo la Wingwi, Wilaya ya Micheweni na kueleza kuwa ujenzi wa skuli hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba shule hiyo ni mojawapo ya miradi iliyojengwa kama ziada ya utekelezaji mzuri wa ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Wakati uo huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Maji tayari imetoa pampu itakayofungwa katika eneo la kilindini na itasafirishwa kesho kwenda kisiwani Pemba.

Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ili kuhakikisha kila liloahidiwa na CCM linatekelezwa kwa wakati, ufanisi, ufasaha, ubunifu na maarifa zaidi.



Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *