KESI dhidi ya
Rais Donald Trump kuhusu utumiaji mbaya wa madaraka na kuzuia Bunge kutekeleza
kazi zake inafikia ukingoni Ijumaa pale Baraza la Seneti litakapokutana kuamua
rais ana hatia au la.
Hoja ya Wademokrats kutaka kuletwa
mashahidi ilionekana kushindwa baada ya Warepublikan waliotarajiwa kuungana nao
kubadili mawazo yao na hivyo wachambuzi wanasema huenda kesi ikamalizika Ijumaa
usiku na kumfutia mashtaka rais Trump.
Seneta Mrepublikan Lamar Alexander,
aliyetarajiwa kuleta mabadiliko kwenye kesi hiyo, alitangaza jana kwamba
hataunga mkono hoja ya kuruhusu mashahidi na kuvuruga matumaini ya Wademokrats
kupata wenzao watatu tu kufikia kura 51 zinazohitajika kuruhusu mashahidi na
kesi kuendelea.
Hivi sasa zinahitajika theluthi
mbili za kura katika Baraza la Seneti kumuondoa rais jambo ambalo
halitawezekana na hivyo kuna uwezekano mkubwa hatopatikana na hatia na kesi
kumalizika.
Wachambuzi hivi sasa wanasema
Wademokrats wanataka kuhakikisha kwamba Trump hatachukuwa uamuzi huu kuwa ni
ushindi kwani wamedhihirisha alifanya makosa.
-VOA
No comments:
Post a Comment