RAIS MAGUFULI AKISAJILI LAINI YAKE NA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA BW. MNAKU ALIYEFARIKI…! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 27 December 2019

RAIS MAGUFULI AKISAJILI LAINI YAKE NA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA BW. MNAKU ALIYEFARIKI…!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole katika  kampuni ya simu ya Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali na Wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao  leo Desemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao  leo Desemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiliamali wa Chipsi  Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment