KATIBU MKUU MWALUKO ATETA NAMKUU WA MKOA MWANZA MAANDALIZI SHEREHE ZA UHURU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 5 December 2019

KATIBU MKUU MWALUKO ATETA NAMKUU WA MKOA MWANZA MAANDALIZI SHEREHE ZA UHURU

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella walipokuwa wakikagua shughuli za maandalizi za  siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimueleza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella,   juu ya umuhimu wa kukamilisha  kwa wakati  shughuli zitakazo fanyika siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe hizo leo, tarehe 5 Desemba, 2019.

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo  leo, tarehe 5 Desemba, 2019 akishuka  katika jukwaa la Uwanja wa CCM  Kirumba, mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi za  Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya   siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.

Kikundi cha Kwaya cha MVC kikifanya  mazoezi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.

No comments:

Post a Comment