BENKI ya NMB imepokea kibali cha ithibati kuwa
mwajiri aliyeidhinishwa na Chama cha Wahasibu cha Kimataifa ‘Association of
Chartered Certified Accountants’ (ACCA) katika kutoa maendeleo stahiki ya taaluma kwa wafanyakazi.
Utambuzi huu unamaanisha kwamba Benki ya
NMB ina kiwango cha kimataifa cha kutoa fursa za wafanyakazi kujiendeleza kitaaluma
na kuamini kuwa mafunzo hayo husaidia
wanachama wa ACCA kwenye benki na taaluma nyingine kukidhi mahitaji yao ya
uzoefu wa vitendo makazini.
NMB walipokea utambuzi huo kutoka ACCA mwishoni
wa mwaka huu, ambapo NMB inakuwa miongoni mwa taasisi 13 nchini na taasisi za
kimataifa zisizopungua 7,000 duniani zinazotambuliwa na ACCA.
NMB na ACCA zitaendelea kuhakikisha
wafanyakazi wanakuzwa kwa viwango vya juu zaidi. Ambapo NMB itaendeleza kuweka
mazingira mazuri na rafikii ya kufanya
kazi ili kusaidia wanachama na wanafunzi
wa mafunzo ya ACCA kupata mafunzo stahiki.
Akizungumza katika mahojiano maalumu,
Meneja mwandamizi Idara ya Ukaguzi wa ndani NMB, Gaudence Nganyagwa, amesema ni
wakati sasa wa Tanzania na Ulimwengu kufahamu jinsi gani NMB inathamini
wafanyakazi wake kwa kuwajengea uwezo ili kuwa wenye ushindani katika kutoa
huduma bora yenye weledi wa kimataifa.
“Tunaamini kuwa ni wakati wa kuifanya
Tanzania na Ulimwengu ujue ni kwa kiasi gani NMB tunathamini maendeleo ya
wafanyakazi wetu. Kwa miaka mingi, benki imekuwa ikiwekeza katika mafunzo na
kuwaendeleza wafanyakazi ili kuzalisha kilicho bora sokoni.
“Tunaamini kwamba kwa ACCA kutupatia tuzo
hii, imethamini na kutambua juhudi zetu za kujitolea katika kuwajengea uwezo
wafanyakazi. Tunaamini kuwa kama viongozi katika tasnia ya huduma za kifedha,
ni jukumu letu kuhamasisha taasisi zingine kuwekeza katika stadi za
watu.”amesema Nganyagwa.
Naye Mkaguzi wa Ndani wa NMB, Sulemani Manyiwa amesema
faida kubwa kwa NMB kuwa mwanachama wa ACCA ni kuifanya NMB kuwa na mwonekano
wa kimataifa.
“Kuwa mwajiri aliyeidhinishwa wa ACCA
kunaboresha mwonekano wa benki
kimataifa. Ni rahisi kwa NMB kuajiri na kuendeleza vipaji bora katika
soko. NMB sasa inaweza kutangaza nafasi mbalimbali kimataifa kupitia tovuti za kazi za ACCA na kushiriki
katika maonesho ya kazi kimataifa.
“Hii pia itafungua milango hata kwa Watanzania
wanaoishi nje ya nchi au wageni wanaotaka kuendeleza kazi zao na mwajiri
aliyejitolea nchini Tanzania. Tafiti zetu na dodoso sasa zitashughulikiwa na
ACCA ili kuongeza ufahamu wa kitaalam kwa mustakabali wa tasnia. Pia tutapigwa
msasa wa mara kwa mara na mwelekeo wa tasnia nakufanya tafiti na matukio ya
pamoja na ACCA.”amesema.
Akithibitisha kuwa nafasi ya kujiendeleza
kielimu na kitaaluma kwa wafanyakazi wa NMB ni ajenda nyeti na ya kimkakati,
Kaimu Ofisa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay aliongeza kuwa
uwekezaji wa benki katika kuendeleza wafanyakazi ni uwekezaji makini ambao
utahakikisha benki ya NMB inaendelea kuwa benki bora katika kuvutia vipaji na
kuviendeleza.
“Benki pia itapata huduma bora zaidi na za harakakutoka
kwa ofisi ya ACCA ya Tanzania kuhusu suala lolote. Wanachama waliohitimu
mafunzo ya ACCA ambao ni wafanyakazi wa NMB watakuwa na uhakika wa kutunza
uanachama wao, na wataweza kujiendeleza na fursa mbalimbali za ACCA katika
gharama ndogo zaidi,” amesema.
ACCA inafanyakazi katika nchi 179 ikiwa
na dhamira ya kuwa kiongozi wa ulimwengu
katika kuunda na kuimarisha uwezo na utendaji wa uhasibu kote ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment