App ya ADA |
Matumizi ya App ya ADA katika simu |
Simu yako daktari wako....! |
Na Mwandishi Wetu
TAKRIBANI watu zaidi ya milioni 100 wanaotafuta huduma za
afya nchi za Afrika Mashariki wanatarajia kunufaika na Programu ya kwanza ya
kishwahili yenye uwezo wa kutathmini dalili za magonjwa inayoendeshwa na akili
bandia (“AI”).
Programu hiyo iliyozinduliwa kwa ushirikiano na Shirika la
Fondation Botnar la Uswisi, Global Health Initiative – ADA pamoja na Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) cha jijini Dar Es Salaam,
Tanzania inatarajiwa kuwa mkombozi kwa jamii hasa za kipato cha chini na kati.
Taarifa zaidi za wadau wa program hiyo zinaeleza kuwa inawezesha
upatikanaji wa taarifa za afya na ushauri App, iliyokuzwa na Ada Health,
inachanganya hifadhidata ya maarifa bora zaidi ya kitiba duniani na teknolojia
erevu ya fikra ili kuwasaidia watumiaji kuelewa nini kinaweza kuwa
kinasababisha dalili zao, na pia kuwapa mwongozo maalum kuhusu wanachotakiwa
kufanya baada ya hapo.
Programu hiyo ‘app’ inakusudia kuwawezesha wagonjwa kupata
taarifa juu ya kinachowasumbua baada ya kuingiza dalili za ugonjwa kisha kufanya
maamuzi kuhusu afya zao, huku ikisaidia kutoa huduma za afya zilizopo, madaktari,
na kliniki. Ulimwenguni kote kuna watu bilioni 4 - zaidi ya nusu ya idadi ya
watu duniani - hawawezi kufikia huduma za msingi za afya.
“Watu bilioni nne duniani kote hawawezi kufikia huduma za
msingi za afya, na nchi nyingi zikiwemo Tanzania, Kenya, Somalia na Msumbiji
zina daktari chini ya 1 kwa watu 1,000 ,” 2 alisema Hila Azadzoy, Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Health Initiative ya Ada.
Bi Azadzoy anabainisha; “Kutokana na upokeaji mpana wa
teknolojia ya kidijitali, kuna fursa kubwa kwa AI kusaidia kushughulikia hili
suala [upungufu wa wahudumu wa afya] kwa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa
wagonjwa na kuwawezesha madaktari kuwa na athari kubwa zaidi kadri
iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Magonjwa ya Watoto wa Chuo Kikuu
cha Muhimbili Cha Afya na Sayansi Shirikishi anasema ili kuwa na ufanisi,
teknolojia hizi lazima zirekebishwe kulingana na hali za kitiba, kitamaduni, na
kilugha katika kila eneo.
Anasema Chuo Kikuu cha Muhimbili kimesaidia maboresho kwa
app hiyo ya Kiswahili. “…Tutakuwa tunaendelea kushirikiana na wataalamu wa
ndani ya Afrika Mashariki kugundua njia zaidi za kuweza kuboresha uwezekano wa
kufikia huduma za afya.”
“Kuna upungufu mkubwa katika huduma za afya ndani ya Afrika
Mashariki na itakuwa vigumu sana kushughulikia suala hili kwa kuongeza idadi ya
wafanyakazi wa afya na madaktari tu. Tunaweza kutatua hili tatizo na kufanya
kila familia iweze kufikia huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa,”
alisema, Dk. Salim.
Naye Mkuu Mtendaji wa Fondation Botnar, Dk. Stefan Germann alisema
wamefanikisha marekebisho kulingana na magonjwa na dalili zilizoenea zaidi eneo
hili, tunapiga hatua muhimu katika kuwaongoza mamilioni ya watu kwenye kutafuta
matibabu. AI ina uwezo mkubwa wa kusaidia kuboresha ufanisi na ubora wa mifumo
yetu ya afya kupitia huduma ya kibinafsi na ya ubashiri zaidi; tunaamini ni
muhimu kwamba faida hizi zinapatikana kwa kila mtu, ulimwenguni kote.
Kasoro za changamoto hii ya afya inawaathiri zaidi watu
kwenye nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Afrika Mashariki ni ukanda
ambao umeathiriwa sana na suala hili. Kwa kutoa programu ya kitiba ya tathmini
ya dalili inayoendeshwa na akili bandia kwa Kiswahili, lugha ambayo inatumiwa
na zaidi ya watu milioni 100 kwenye nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda,
Msumbiji, mpaka Somalia, Ada inatumaini kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa
kufikia taarifa bora za afya na ushauri, haswa kwa vijana na familia. Toleo la
Kiswahili la app ya Ada limekuzwa kama sehemu ya Mpango wa Afya Duniani,
“Global Health Initiative (GHI)” wa Ada.
Huu ni mpango wa muda mrefu wenye lengo la kukabiliana na
upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya - ambao unatarajiwa kufikia zaidi
ya milioni 12.9 ifikapo mwaka 2035. Ada inakabiliana na upungufu huu katika
huduma za afya.
Dk. Germann, anaongeza kuwa App kama ya Ada inaweza
kuwafanya wagonjwa, haswa vijana, kuwa wadau wenye ufahamu juu ya afya zao.
Hivyo basi, kuunda vifaa vya afya vya kidijitali maalumu kwa matakwa na
mahitaji ya eneo husika katika nchi za kipato cha chini na cha kati ni muhimu
katika kufikia usawa kwenye upatikanaji wa huduma za afya.” aliongeza kusema, “Tunajivunia kuzindua toleo la Kiswahili la app ya Ada na tunatarajia
kushirikiana zaidi ili kutekeleza maono yetu ya pamoja ya kutumia teknolojia
kusaidia wagonjwa, bila kujali wanaishi wapi.”
Kuchanganya akili bandia, utaalamu wa matibabu ya kibinadamu
na nguvu ya teknolojia ya kidijitali ili kufikisha huduma za afya na mwongozo
kwa wengi. Washirika wa Ada katika kuikuza na kuifanya app iendane na mazingira
ya Afrika Mashariki ni shirika la Fondation Botnar la Uswisi, ambalo ni shirika
lililojikita kwenye kutumia teknolojia ili kuboresha afya na ustawi wa vijana
katika nchi za kipato cha chini na cha kati.
App inapatikana kupitia simu zote za iOS na Android.
Kurekebisha AI za Ada kuendana na changamoto za kipekee za kiafya za Afrika
Mashariki Ada imefanya kazi na washirika wenyeji, madaktari na mashirika ya
afya ili kuhakikisha app inarekebishwa kuendeana na isimu ya lugha, utamaduni
na maudhui ya kitiba ya kila eneo.
No comments:
Post a Comment