Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, leo Novemba 23, 2019 amewaapisha Wajumbe wa
Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni na Temeke.
Kwa upande wa
Wilaya ya Kionondoni, walioapishwa ni pamoja na Bw. Derek Murusuri, Balozi Celestine Christopher Liundi na Mama
Merina Mlunde.
Aidha Mheshimiwa
Makonda pia aliwaapisha wajumbe wengine wane wa Wilaya ya Temeke.
Akitoa nasaha
zake baada ya zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda aliwataka Wajumbe hao
kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro na sio kuichochea.
Aliwataka
Wajumbe hao kutumia mbinu zote kutatua migogoro ya ardhi ili mashauri yasiwe
yanachukua muda mrefu.
"Muwe msaada kwa watu wote na hasa wanyonge, wajane na yatima ili
wapate haki yap," alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimuapisha Bw. Derek Murusuri kuwa Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni.
Mhe. Makonda akimkabidhi kitendea kazi Bw. Murusuri mara baada ya kumuapisha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul makonda (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Abubakar Kunenge (wapili kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe hao baada ya kuwaapisha.
No comments:
Post a Comment