Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene. |
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, watapamba maonesho ya Siku ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu Tanzania yanayoanza Ijumaa Novemba 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Taarifa zaidi zinaeleza,
maonesho hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania
(TAREA) kwa ufadhili wa taasisi za Kingdom of The Netherland, Energy Plus,
Brac, Chloride Solar, Solar Sister na Ewura. TAREA ni jumuiya yenye
wanachama zaidi ya 796.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Makamu Mwenyekiti wa TAREA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Maonesho hayo, Mhandisi Prosper Magali alisema maonesho hayo
yatafanyika Ijumaa Novemba 29 na Jumamosi Novemba 30, mwaka huu katika Viwanja
ya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani. |
“Maonesho yatafunguliwa
Ijumaa na Waziri mwenye dhamana ya Mazingira, George Simbachawene na
kufungwa Jumamosi na Waziri wa Nishati, Dk Kalemani atakayemwakilisha
Waziri Mkuu,” alisema Magali na kuongeza: “Wadau na watu mbalimbali wajitokeze
kwa wingi kushuhudia teknolojia ya renewable energy (nishati jadidifu) kwa kuwa
licha ya mambo mengi mazuri yatakayofanyika na kuoneshwa, hakuna kiingilio.”
Aidha, Mhandisi Magali
alisema lengo la Maonesho hayo yenye kaulimbi isemayo: “NISHATI JADIDIFU
KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA,” ni kuionesha jamii namna Nishati Jadidifu
inavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo Mwaka
2025.
“Maonesho
yatahusisha Teknolojia ya Nishati Jadidifu, Kutembelea Maeneo Yanayotumia
Nishati Jadidifu kuona teknolojia hii inavyofanya kazi, pamoja na warsha na
majadiliano ya kitaalamu,” alisema.
KUHUSU PICHA, TAARIFA NA
MAELEZO ZAIDI, bonyeza hapa; https://sites.google.com/site/tareatzevents/red2019
No comments:
Post a Comment