RAIS DK MAKUFULI AFUNGUA BARABARA YA TUNDUMA –SUMBAWANGA KM 223.21 KATIKA ENEO LA LAELA MKOANI RUKWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 6 October 2019

RAIS DK MAKUFULI AFUNGUA BARABARA YA TUNDUMA –SUMBAWANGA KM 223.21 KATIKA ENEO LA LAELA MKOANI RUKWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia aliyeshika utepe, viongozi wa mkoa wa Rukwa, Mawaziri, viongozi wa Dini pamoja na Chama, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.


Sehemu ya Barabara ya Tunduma –Sumbawanga km 223.21 iliyofunguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Laela mkoani Rukwa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Laela mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chiwanda Tunduma mkoani Songwe mara baada ya kusimama wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na maaskari wa Jeshi la Polisi wakati akielekea kukagua kituo cha polisi cha Laela mkoani Rukwa mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali waliojipanga pembezoni mwa barabara Kuu ya Tunduma Sumbawanga mara baada ya kutoka Laela kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Wananchi wa Ikana wakisangilia mara baada ya kumuona  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye eneo hilo wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.




No comments:

Post a Comment