BENKI ya NMB imetoa msaada wa madawati 215 katika shule za
sekondari Mahenge, Vigoi na Isongo zilizoko wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro na
Ng’hoboko iliyoko wilayani Meatu Mkoani Simiyu.
Mbali na hilo benki hiyo pia imetoa msaada wa vifaa tiba
katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto vyenya thamani ya shilingi milioni tano
ambapo vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na
vitanda na mashuka na magodoro.
Msaada huo wa madawati umegharimu kiasi cha sh. Milioni 20,
ambapo katika shule za Wlaya ya ulanga benki hiyo imetoa madawati 165
yaliyogharimu Milioni 15 huku katika shule ya Ng’hoboko imetoa madawati 50
ambayo yamegharimu Milioni 5.
Vifaa hivyo pamoja na madawati vimetolewa kwa nyakati
tofauti ndani ya wiki hii, ambapo vinaifanya benki hiyo kuchangia katika shughuli
za maendeleo jumla ya shilingi Milioni 675 hadi sasa kwa mwaka huu tu.
Meneja wa benki hiyo kanda ya Magharibi Sospeter Magesse
akiongea katika hafla ya kukabidhi madawati shule ya Ng’hoboko alisema kuwa
msaada huo umetolewa ili kuwawezesha wanafunzi wasome vizuri.
Alisemakuwa benki hiyo imekuwa ikitenga kiasi cha sh.
Bilioni moja kila mwaka kwa ajili ya kurejesha kwa wananchi, pesa ambayo
imekuwa ikitumika kuboresha huduma za elimu, na afya.
“NMB kama benki ya watanzania itaendelea kusaidiana na serikali
pamoja na watanzania katika kuboresha huduma za afya na elimu, tuna imani kwa
msaada huu wanafunzi watajisomea vizuri,” alisema Magesse.
Naye Nsolo Mlozi Meneja wa benki hiyo kanda ya kati
akikabidhi vifaa tiba katika hospiali hiyo alisema kuwa NMB inatoa msaada huo
kama njia ya kurudisha faida kwa wananchi ambao ndiyo wateja wao wakubwa.
“Ingawa Serikali inafanya makubwa, Benki hiyo inao wajibu wa
kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kwa kusaidia jamii kwani kupitia jamii
hii hii, ndio imeifanya benki NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote
hapa nchini,” Alisema Mlozi.
“Vifaa hivi vya tiba na afya tunavyokabidhi leo ni moja ya
ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania
tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,”
aliongeza Mlozi.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Ngolo Malenya akipokea madawati ameishukuru benki ya
NMB kwa kutoa madawati 165 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za
sekondari za mahenge ,vigoi na isongo.
Ametoa wito kwa wanafunzi hao kuwa mabalozi
kwa wazazi wao kwa kuwaeleza mambo mazuri yanayofanywa na benki hiyo ili pia wazazi hao waiunge mkono
benki hiyo kwa kufungua account
mbalimbali ili NMB izidi kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kuleta
maendeleo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Chilongani
aliishukuru benki ya NMB huku akitaka wanafunzi wa shule hiyo na walimu
kuhakikisha madawati hayo yanatunzwa ili kudumu kwa muda mrefu.
“Kuna haja ya kuweka adhabu kidogo kwa wale ambao watahusika
kuaribu haya madawati, akiaribu mwanafunzi yeye au mzazi wake wahusike katika
kutengeneza, tunataka haya madawati yatumiwe na wadogo zetu ili waone umuhimu
wa NMB,” Alisema Chilongani.
No comments:
Post a Comment