Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Siporah Liana (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam. |
Ofisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akizungumza na wateja (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa maadhimisho Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam. |
Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City akitoa shukrani kwa benki hiyo kwenye uzinduzi wa maadhimisho Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam. |
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Irine Masack akiitambulisha timu inayowahudumia wateja katika tawi hilo. |
Baadhi ya wateja wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika Tawi la NMB, Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
BENKI ya NMB imeongeza muda wa kufanya kazi kwa baadhi ya
matawi yake ikiwa ni sehemu ya maboresho ili kuhakikisha wateja wake wanapata
huduma kwa ufasaha. Kwa kuanzia mwezi huu matawi ya NMB Kongo, NMB Mlimani City
na Kahama Business Centre yatafanya kazi hadi saa moja jioni.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho Wiki ya Huduma
kwa Wateja, Ofisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema kuanzia
mwezi Oktoba matawi yaliotajwa yatakuwa yanafunguliwa saa nne asubuhi na
kufungwa saa moja jioni.
Mbali na mabadiliko hayo, NMB pia imeongeza muda wa
kuhudumia wateja kwa kitengo chetu cha Huduma kwa Wateja, badala ya kufunga saa
nne usiku, kuanzia mwezi huu kituo hicho kitakuwa kinafungwa saa sita kamili
usiku.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar
es Salaam, Bi. Siporah Liana aliipongeza NMB Benki kwa maboresho inayoyafanya
kwani yanazidi kuwavutia wateja wengi. Aliipongeza benki hiyo kwa huduma za
kijamii ambazo imekuwa ikijitoa katika nyanja za elimu, afya na majanga mengine
yanayojitokeza kwa jamii yetu.
"...Mnafanya mambo makubwa kwa jamii, nimeona kuna
sehemu unajitolea madawati na viti kwa shule, vifaa tiba katika hospitali na
vituo vya afya na mnasaidia kwenye majanga tunawahakikishia mchango wenu
unaonekana kwa jamii endeleeni kuisaidia," alisema Bi. Siporah Liana.
Awali akizungumza, Bi. Zaipuna alibainisha kuwa kwa sasa
huduma za NMB zipo kwa kila wilaya huku ikijivunia kutoa huduma nafuu zaidi.
"...Mpaka sasa tuna matawi 230, ATM Zaidi ya 800 na NMB Wakala Zaidi ya
6000. Ndugu Mgeni Rasmi, maboresho haya yote situ kwaajili ya mwezi huu wa
huduma kwa wateja, bali ni endelevu." Alisema ofisa huyo mwandamizi wa
NMB.
Mwezi wa 10 kila mwaka,dunia huadhimisha Wiki ya Huduma kwa
Wateja. Kwa NMB siku hii tunaichukulia kama fursa muhimu ya kuendeleza maono ya
benki – Kumjali Mteja katika matawi yetu yote.
No comments:
Post a Comment