|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza alipokuwa akifunga warsha ya wanahabari juu ya mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi oktoba hadi disemba 2019 iliyofanyika leo Makao Makuu ya TMA. Kulia ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa. |
|
Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa akifafanua jambo kwenye warsha hiyo ya TMA kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari. |
|
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri - TMA, Bw. Samwel Mbuya akifafanua jambo katika warsha hiyo kwa wanahabari leo. Kulia ni Dk. Agnes Kijazi. |
|
Mmoja wa wataalam kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (kulia) akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo. |
|
Ofisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni (kushoto) akifafanua jambo katika warsha hiyo kwa wanahabari. |
|
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akizungumza. |
|
Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo. |
|
Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa warsha hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi mara baada ya kufunga warsha hiyo. |
MAMLAYA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imefanya warsha kwa waandishi wa habari mbalimbali juu ya mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi oktoba hadi disemba 2019. Warsha hii ni muendelezo wa juhudi za mamlaka kutaka kuhakikisha taarifa zake hasa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika na usahihi zaidi.
Akifunga warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema taarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii kwa haraka, uhakika na usahihi zinasaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na pia zinasaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango ya kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa, upatikanaji wa chakula na lishe bora pamoja na afya kwa ustawi wa jamii.
"...Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu hii ya tano inatambua vyema mchango mkubwa wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa kuwafikia wananchi wote kwa wakati. Hivyo basi ili kudhihirisha hilo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imekuwa ikihakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla na kuwaelimisha zaidi.
Alibainisha kuwa lengo kuu la warsha hiyo ilikuwa kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2019 na athari zinazoweza kujitokeza. Katika warsha hiyo wataalamu wa TMA waliwasilisha rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri mpya wa mwezi Oktoba hadi Disemba 2019, na kujadili pamoja na wanahabari kabla ya kupata uelewa wa pamoja na kurahisisha uwasilishwaji wake kwa jamii katika lugha inayoeleweka.
Hata hivyo, Mamlaka imekuwa na uhusiano mkubwa sana na vyombo vya habari kwa kipindi kirefu sasa, na pia warsha hizi zimekuwa zikifanyika mara kwa mara kabla ya kutolewa kwa mwelekeo wa msimu wa mvua za masika na vuli.
No comments:
Post a Comment